Waziri mkuu Mizengo Pinda

Waziri mkuu Mizengo Pinda

Waziri mkuu Mizengo Pinda amewataka wanasiasa kuepuka matamshi na vitisho vinavyohamasisha wananchama wao kujenga chuki na uhasama kwa serikali iliyopo madarakani.

Akiahirisha mkutano 10 wa bunge mjini Dodoma amesema vitendo hivyo vinavyokwenda kinyume na sheria, endapo vitaachiwa vinaweza kuwagawa watanzania.

Pinda amesema ni muhimu kwa watanzania kujenga mazingira ya kuvumiliana katika kujenga demokrasia ya kweli nchini

Aidha waziri mkuu Pinda amewataka viongozi wa dini kusaidia utatuzi wa migogoro inayojitokeza ndani ya jamii na kuondokana na kauli za kashfa dhidi madhehebu mengine ya dini.

Amesema madhehebu ya dini yana nafasi ya kujenga umoja na mshikamano, hivyo amewaomba viongozi hao kutatua kwa amani migogoro iliyopo na kuwaelimisha wafuasi wao kuthamani amani.

Amesema serikali imetoa uhuru wa kuabudu dini inayotaka hivyo hakuna haja ya dini moja kukashifu dini nyingine.

Advertisements