Benki ya Kislamu Zanzibar imezitaka taasisi za kislamu zikiwemo madrasa na vyuo vya Qur-ani kutumia fursa ya mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa na benki hiyo kwa ajili ya shughuli zao za maendeleo.

Wito huo umetolewa na kaimu mkurugenzi mtendaji wa benki ya kislamu PBZ Mohammed Halfan Tahir katika hafla ya kukabidhi msaada wa mifuko ya saruji 80 kusaidia ujenzi wa madras Munawar ya Malindi.

Amesema huduma ya mikopo hiyo inayotolewa kwa taratibu na sheria za kislamu itazisaidia taasisi hizo hasa vyuo vya qur-ani na madrassa katika ujenzi wa majengo yao pamoja na kuanzisha miradi ya kiuchumi.

Aidha Zahor amesema benki ya Kislamu imekuwa ikitumia faida yake kusaidia miradi ya kijamii.

Nae mkuu wa Madrassa Munawar Abeid Mahafoudh ameishukuru benki hiyo kwa msaada wake huo na kuziomba taasisi nyingine kusaidia maendeleo ya madrassa hiyo.

Madrassa ya Munawari iliyoanzishwa zaidi ya miaka 60 ina wanafunzi wapatao 500.

Advertisements