maitiMaelfu ya waislamu leo wamehudhuria maziko ya mwanazuoni Sheikh Nassor Abdalla Bachoo aliefariki jana baada  ya kuugua kwa muda mrefu huko kijijini kwao Donge.

Awali kabla ya maziko hayo kulitokea sitofahamu ya eneo la kuzikiwa shehe huyo kufuatia baadhi ya wanafamilia kutaka kuzikwa mbele ya kibla cha msikiti, lakini wanafunzi wake walikataa na hatimae kuzikwa katika eneo jingine.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni   makamu wa kwanza wa rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wengine wa taasisi za kidini, serikali na vyama vya siasa.

Awali mwili wa Shekhe Bachoo ulisaliwa  na umati wa watu katika viwanja vya Mnazi mmoja na baadae kuelekeaa Donge kwa ajili ya maziko.

Sheikh Nassor Bachoo alianza kuugua mwaka mmoja uliopita ambapo mwishoni mwa mwaka 2012 alipelekwa India kwa ajili ya matibabu zaidi.

Wakati akiugua na kupatiwa matibabu, Sheikh Bachoo aliwahi kuzushiwa kifo zaidi ya mara tatu na kusababisha mwanawe kuanza kutoa taarifa katika vyombo vya habari kukanusha taarifa hizo

Advertisements