Padri Evaristy Mushi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Parokia ya Beilt Ras Viswani Zanzibar

Padri Evaristy Mushi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Parokia ya Beilt Ras Viswani Zanzibar

Watu waliokuwa na bunduki leo wamempiga risasi na kumuuwa padri mmoja wa kanisa Katoliki katika kisiwa cha Zanzibar, likiwa ni shambulizi la pili kuwahi kufanywa katika miezi ya karibuni katika kisiwa hicho ambacho idadi kubwa ya wakaazi wake ni Waislamu. Msemaji wa polisi kisiwani humo Mohammed Mhina amesema Kasisi Evarist Mushi alizuiwa na vijana wawili nje ya  lango la kanisa , kabla ya mmoja wao kumpiga risasi kichwani. Mhina amesema kwa sasa kiini cha shambulizi hilo hakijajulikana, lakini polisi inafanya msako wa kuwanasa majambazi hao. Mnamo siku ya Krismasi, watu waliokuwa na bunduki  walimpiga risasi na kumjeruhi vibaya kasisi wa kikatoliki wakati akirejea nyumbani kutoka kanisani. Haijabainika kama mashambulizi hayo mawili yanahusiana, au  ikiwa yamechochewa na hisia za kidini. Mwezi Novemba mwaka jana, washambuliaji walimmwagia kemikali usoni na kifuani mhubiri mmoja wa kiislamu, na kumekuwa na hofu baina ya jamii hizo mbili kisiwani Unguja

CCM ATAOA RAMBI RAMBI:

Chama Cha Mapinduzi kimeelezea kusikitishwa kwake na tukio la kinyama lililofanywa na watu wasiojulika kumpiga risasi na kumuua Padri Evaristy Mushi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Parokia ya Beilt Ras Viswani Zanzibar leo asubuhi.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamti Maalum ya MNEC Zanzibar Idara ya Itikadi na Uenezi Waride Bakari Jabu akilitaja tukio hilo na mengine yakijumuishwa katika orodha yavitendo vya ukatili na uhalifu kunakoongeza taharuki Zanzibar.

Waride amesema mfululizo wa mashambulizi kwa viongozi wa dini kunazidi kuijengea taaswira chafu Zanzibar huku watuhumiwa wa matuklio hao bado wakiwa hawajawakamatwa na kufikishwa mbele ya mikono ya sheria.

Aidha Chama Cha Mapinduzi kwa upande wake kimeyataja matukkio hayo kuwa ni sehemu ya ukatili unaotisha ,ukijenga sintofahamu, kuleta mgawanyiko na kuathiri mashirikiano, umoja wa kitaifa na sifa njema ya visiwa hivyo.

Msemaji huyo wa CCM Zanzibar ameviomba vyombo vya upelelezi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha vinachukua hatua ya kudhibiti matukio hayo, kuwakamata watuhumiwa na kujua chimbuko la uharamia huo.

Waride amesema ukimya wa vyombo vyenye dhamana ya upepelezi na uchunguzi dhidi ya matukio yanayowaandama viongozi wa dini kunazidi kukatisha tamaa na kutotoa picha halisi.

Katibu huyo wa Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar ameyataja matukio ya mara kwa mara yanayotokea yakiwemo ya nyumba za ibada kuchomwa moto,kiongozi wa kiislam sheikh Fadhil Sotraga kumwagiwa tindikali, Padri Ambrose Mkenda kujeruhiwa kwa risasi na sasa Pdri Mushi kuuawa, hakuiletei muonekano mwema Zanzibar.

Waride ameeleza kuwa vitendo hivyo vimekosa kujali na kuthamini thamani ya utu huku vikikiuka ustaarabu uliozooeleka na kwamba CCM inalaani viakali kushamiri kujitokeza kwa uhalifu na uharamia visiwani Zanzibar,.

Chama Cha Mapinduzi kimetoa wito na kuwaomba wananchi , viongozi wa kiroho na waumini wa dini mbalimbali kuwa na ustahamilivu hivi sasa huku vyombo vyenye dhamana vikifanyan kila linalostahili kuwatia nguvuni wahusioka wa matukio hayo kwa mujibu wa sheria

Advertisements