Maalim Seif akihutubia mikoa miwili ya Pemba Gonbani.

Maalim Seif akihutubia mikoa miwili ya Pemba Gonbani.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ameihimiza Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuendelea kusimamia uadilifu katika hatua zote za mchakato wa kupata katiba mpya, ikiwemo kuhakikisha Masheha wanatenda haki katika hatua hii ya kupata wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.
Maalim Seif ameyasema hayo wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa CUF wa mikoa miwili ya Pemba, uliofanyika huko katika uwanja wa Gombani ya Kale, Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba. Amesema kuwa baada ya kukamilika kwa hatua za kutunga sheria ya Tume na baadaye kukusanya maoni ya wananchi, hivi sasa wananchi mbali mbali wameomba kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, hatua ambayo inawahusisha Masheha kwa upande wa Zanzibar. “Ni imani yangu Masheha watatangaza majina ya watu wote waliomba kuwa wajumbe wa Mabaraza ifikapo tarehe 22, na Tume ya Jaji Warioba inawajibu wa kuhakikisha hakuna ubabaishaji katika hatua hii”, alisema Katibu Mkuu wa CUF.
Alisema kuwa Tume ya Mabadilika ya Katiba lazima ihakikishe haki inatendeka na haina budi kujiepusha na kuwaachia Masheha kufanya watakavyo, kwa vile kitendo kama hicho kinaweza kusababisha baadhi ya watu wasitendewe haki.
Maalim Seif aliwapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuweza kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao, wakati zoezi la kuchukua maoni lilipokuwa likiendelea na kuitaka Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo hivi sasa imo katika kuyapitia maoni ya wananchi kabla ya kutoa rasimu, kiyazingatia matakwa ya wananchi walio wengi.
Alieleza kuwa kilichojitokeza wakati wa zoezi la kuchukua maoni, wananchi walio wengi wa Zanzibar walitaka Zanzibar iwe na mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yake, na hivyo matarajio yake rasimu ya katiba itakayotolewa na Tume kwa ajili ya kujadiliwa itazingatia maoni hayo.  
Mapema katika risala yao, wanachama wa CUF katika mikoa miwili ya Pemba wameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyo chini ya mfumo wa Umoja wa Kitaifa, kwa kuendelea kudumisha amani na umoja wa Wazanzibari, na kuhimiza baadhi ya viongozi na wananchi wachache ambao wameonesha kutofurahia hali ya maelewano wazidi kuelimishwa ili waelewe

Advertisements