Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Zanzibar Sheha Mjaja Juma kuhusiana na hatua iliyofikiwa juu ya mradi wa maji safi na salama katika Shehia ya Kilimani Jimbo la Nungwi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Zanzibar Sheha Mjaja Juma kuhusiana na hatua iliyofikiwa juu ya mradi wa maji safi na salama katika Shehia ya Kilimani Jimbo la Nungwi

Marekani imemteua Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Abdulhabib Fereji kuwa ni kati ya wanawake wawili jasiri Tanzania katika mwaka 2013.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini imesema kutokana na kuteuliwa huko, Waziri Fereji atakabidhiwa tunzo maalum ya Mwanamke jasiri (Tanzania Women of Courage Award) kutoka Ubalozi wa Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Jefferson Smith Machi 13,  Tuzo hiyo itatolewa April 4, mwaka huu huko ofisi za Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, jijini Dar es Salaam.
“Nakupongeza kwa kuwa kati ya wanawake wawili walioteuliwa kupokea Tuzo ya Mwanamke jasiri 2013, Balozi Alfonso Lenhardt anakukaribisha kuja kupokea tuzo hiyo katika ofisi za Ubalozi April 4”, ilisema barua ya Ubalozi kwa Mheshimiwa Waziri Fereji.
Taarifa hiyo imesema miongoni mwa sababu za kuteuliwa kwake ni kutokana na mchango wake mkubwa katika kufanikisha ushiriki wa wanawake katika masuala ya siasa, akiwa Mwakilishi wa Kwanza Mwanamke wa kuchaguliwa.
Vigezo vyengine ni mchango mkubwa alioutoa katika kufanikisha maridhiano ya kisiasa Zanzibar, ambayo yamefuta uhasama miongoni mwa wananchi wa Zanzibar mwaka 2009, kusimamia upatikanaji haki za wanawake na watoto, pamoja na kuhimiza na kusimamia utawala bora na uwazi serikalini.
Mwanamke mwengine aliyeteuliwa kupata tuzo hiyo 2013, ni Ndinini Kimesera Sikar, ambaye ni miongoni mwa waanzilishi wa taasisi inayoshughulikia Maendeleo ya Wanawake Wamasai (MWEDO), hasa katika kusimamia elimu, na kuwajengea uwezo wanawake na watoto katika jamii ya Wamasai.

Advertisements