Archive for April, 2013

ZANZIBAR KUJENGA BANDARI MPYA YA MIZIGO

Sehemu ya kupakia mizigo bandari ya Malindi

Sehemu ya kupakia mizigo bandari ya Malindi

WIZARA YA MIUNDO MBINU NA MAWASILIANO BADO INAENDELEA KUMTAFUTA MWEKEZAJI AU MKOPO KWA AJILI YA KUJENGA BANDARI MPYA YA MIZIGO KATIKA ENEO LA MARUHUBI.

            AKIJIBU SUALA KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA WAWAKILISHI NAIBU WAZIRI MH. ISSA HAJI GAVU AMESEMA KAMPUNI KADHAA ZIMEONESHA NIA YA KUTAKA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUWEKEZA MRADI HUO.

            AMESEMA MAJADILIANO NA KAMPUNI HIZO YANAENDELEA ILI KUIPATA KAMPUNI MOJA ITAKAYOSHIRIKIANA NA SERIKALI KWA UTARATIBU WA UJENZI NA UENDESHAJI UTAKAOKUBALIKA.

            SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IMEAMUWA KUJENGA BANDARI MPYA YA MIZIGO KATIKA ENEO LA MARUHUBI KUTOKANA NA UFINYU WA NAFASI KATIKA BANDARI YA MALINDI.

SMZ KUITISHA KURA YA MAONI KUWAICHUA WAFANYABIASHARA WA DAWA ZA KULEVYA

fatmaSerikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema utaratibu wa kuitisha kura ya maoni ya kuwafichua watu wanaouza na kuingiza dawa za kulevya kutoka nje ya nchi unaweza kutumika.

        Hata hivyo waziri wa nchi ofisi ya makumu wa kwanza wa rais Fatma Ferej amesema utekelezaji wa kuitisha kura hiyo inahitaji gharama kubwa.

        Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi amesema dawa za kulevya ni chazo cha vijana kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi, lakini mpango wa kuwafichua watu wanaosambaza na kuuza dawa hizo bado unaendelea.

        Wakati huo huo waziri Ferej amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefanikiwa kudhibiti kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi chini ya asilimia moja tangu mwaka 2002.

        Waziri Ferej amesema hali hiyo inatokana na wananchi kufahamu maambukizi ya ukimwi na athari zake kiuchumi na kijamii.

            Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2012 Zanzibar ina watu elfu sita, 793 wanaoishi na virusi vya ukimwi kutoka watu efu tano, 953 mwaka 2011.

SMZ YAJITAHIDI KULIPIA ADA ZA WANAFUNZI NJE

SHAMHUNAWizara ya elimu na mafunzo ya amali imesema wanafunzi wote wanaosama vyuo vya nje wameshalipiwa gharama ya masomo kwa silimia 75 ikiwemo ada ya masomo, chakula na malazi.

        Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi waziri Ali Juma Shamhuna amesema malipo hayo yanatokana na bodi ya mikopo ya elimu ya juu Zanzibar kuingiziwa shilingi bilioni 4.3.

        Amesema bodi hiyo inatoa umuhimu wa kulipa ada za wanafunzi walioko nje ya Zanzibar kutokana na tatizo la kuzuiliwa masomo yao kwa sababu za kuchelewa kufanya malipo.

        Hata hivyo amewataka wazazi wa wanafunzi hao kuendelea kuwahudumia watoto wao walioko nje ya nchi kwa gharama za chakula na malazi pale fedha za serikali zinapochelewa.

        Waziri Shamhuna amesema serikali inatumia fedha nyingi kuwasomesha vijana nje ya nchi, hivyo imeamuwa kuzuwia wanafunzi wa aina hiyo kwa zile fani ziliopo ndani ya nchi.

        Amefahamisha mwanafunzi mmoja anaesoma udaktari nchini China serikali inagharamika kumlipia zaidi ya dola za Marekani milioni 56.