SHAMHUNAWizara ya elimu na mafunzo ya amali imesema wanafunzi wote wanaosama vyuo vya nje wameshalipiwa gharama ya masomo kwa silimia 75 ikiwemo ada ya masomo, chakula na malazi.

        Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi waziri Ali Juma Shamhuna amesema malipo hayo yanatokana na bodi ya mikopo ya elimu ya juu Zanzibar kuingiziwa shilingi bilioni 4.3.

        Amesema bodi hiyo inatoa umuhimu wa kulipa ada za wanafunzi walioko nje ya Zanzibar kutokana na tatizo la kuzuiliwa masomo yao kwa sababu za kuchelewa kufanya malipo.

        Hata hivyo amewataka wazazi wa wanafunzi hao kuendelea kuwahudumia watoto wao walioko nje ya nchi kwa gharama za chakula na malazi pale fedha za serikali zinapochelewa.

        Waziri Shamhuna amesema serikali inatumia fedha nyingi kuwasomesha vijana nje ya nchi, hivyo imeamuwa kuzuwia wanafunzi wa aina hiyo kwa zile fani ziliopo ndani ya nchi.

        Amefahamisha mwanafunzi mmoja anaesoma udaktari nchini China serikali inagharamika kumlipia zaidi ya dola za Marekani milioni 56.

Advertisements