fatmaSerikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema utaratibu wa kuitisha kura ya maoni ya kuwafichua watu wanaouza na kuingiza dawa za kulevya kutoka nje ya nchi unaweza kutumika.

        Hata hivyo waziri wa nchi ofisi ya makumu wa kwanza wa rais Fatma Ferej amesema utekelezaji wa kuitisha kura hiyo inahitaji gharama kubwa.

        Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi amesema dawa za kulevya ni chazo cha vijana kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi, lakini mpango wa kuwafichua watu wanaosambaza na kuuza dawa hizo bado unaendelea.

        Wakati huo huo waziri Ferej amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefanikiwa kudhibiti kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi chini ya asilimia moja tangu mwaka 2002.

        Waziri Ferej amesema hali hiyo inatokana na wananchi kufahamu maambukizi ya ukimwi na athari zake kiuchumi na kijamii.

            Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2012 Zanzibar ina watu elfu sita, 793 wanaoishi na virusi vya ukimwi kutoka watu efu tano, 953 mwaka 2011.

Advertisements