Archive for June, 2013

AL-HAJJ ABOUD JUMBE ATIMIZA MIAKA 93

jumbeRais Mstaafu awamu ya pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Alhajj Aboud Jumbe Mwinyi leo ametimiza umri miaka 93 ya kuzaliwa.

Alhajj Jumbe amesema anamshukuru mwenyezi Mungu kwa  umri aliyomjaalia  kutokana na kushuhudia neema nyingi.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Ustadh Mohammed Yoyota katika hafla ya kumombea dua huko Kiembesamaki amesema Mwewnyezi Mungu amejalia huruma na hisani alipokabidhiwa dhamana ya kuongoza Zanzibar.

Hata hivyo amesema mwenyezi mungu alimuongoza pale alipoteleza na kumuomba kuitakasa amali yake pamoja na waislamu wenzake ili kuwa na majibu sahihi mbele yake.

Akitowa shukurani kwa waalikwa waliohudhuria dua hiyo mmoja wa mototo wake, Mustafa Aboud Jumbe amesema dua hiyo inatokana na utaratibu wa baba yao kusomewa.

Amesema familia hiyo inapata masuala mengi kuhusu hali ya  baba yao, lakini  amesema hajambo anazungumza na tatizo linalomsumbua ni uzee, nuru ya macho na usikivu.

Rais huyo mstaafu hajaonekana hadharani kwa miaka mingi sasa na anaishi nyumbani kweke Kigamboni mkoani  Dar es Salaam

Advertisements

BOMU JINGINE LARIPUKA ARUSHA NA KUUWA

arusha bomuntenaTaarifa kutoka mjini Arusha zinasema watu wawili wameuwawa na wengine zaidi ya watano wamejeruhiwa baada ya kutoa mripuko unadhaniwa bomu katika mkutano wa hadhara wa chama cha CHADEMA.

Mripuko huo umetokea katika viwanja vya Soweto uliokuwa ukihutubiwa na mwenyekiti wa chama hicho taifa Freeman Mbowe.

Habari zaidi zinasema gari la kubeba wagonjwa la hospitali ya Mount Meru limepasuliwa vioo na wafuasi wa chama hicho wakidai lilichelewa kufika eneo la tukio mpaka watu hao wamepoteza maisha

TANZANIA KUWA NA MFUMO WA SERIKALI TATU NA WAGOMBEA BINAFSI

mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katika tanania  Jaji Joseph Warioba

mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katika tanania Jaji Joseph Warioba

Tume ya mabadiliko ya katiba ya muungano imependekeza kuwepo na mfumo wa serikali tatu ndani ya muungano utakaozijumuisha serikali ya Tanganyika, Zanzibar na serikali ya Jamhuri.

Akizungumza katika kizindua rasimu ya katiba mpya iliyotokana na maoni ya wananchi mjini Dar es Salaam mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Joseph Warioba amesema licha ya wananchi kupendekeza mfumo wa maktaba, serikali nne, mbili, lakini tume imeshawishika na mfumo wa serikali tatu kufuatia maoni hayo.

Warioba amesema tume hiyo haijashawishika na maoni yaliotolewa na wananchi ya kuvunjwa kwa muungano

Amesema katika mfumo huo bunge la muungano litakuwa na wajumbe 75, 20 kutoka Zanzibar, 50 kutoka Tanganyika na watano watakaoteuliwa na rais kutoka kundi la watu wenye ulemavu.

Aidha warioba amesema katika rasimu hiyo tume imependekeza kuwepo wagombea binafsi na vyama vya siasa katika uchaguzi wa urais, ubunge, udiwani na wenyeviti wa vijiji.

Kuhusu ushindi wa kura wa nafasi ya urais tume hiyo imependekeza mgombea wa nafasi hiyo apate zaidi ya asilimia 50 ya kura badala ya mfumo wa sasa wa kura nyingi za mgombea.

Hata hivyo amesema matokeo hayo yanaweza kupingwa na chombo cha mahakama ya juu badala ya mfumo wa sasa wa tume ya uchaguzi ndio yenye mamlaka ya mwisho.

Zaidi ya watu Milioni moja na laki tano waliotoa maoni ya moja kwa maoja, kwa maandishi yakiwemo makundi 160 na maoni ya viongozi wa kitaifa na wastaafu.

Rasimu hiyo ya katiba inatarajiwa kusambazwa kwa wananchi ili kutoa nafasi kwa wajumbe wa baraza ya katiba kuisoma mapema kabla ya kuipitia kwenye mabaraza yao.