mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katika tanania  Jaji Joseph Warioba

mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katika tanania Jaji Joseph Warioba

Tume ya mabadiliko ya katiba ya muungano imependekeza kuwepo na mfumo wa serikali tatu ndani ya muungano utakaozijumuisha serikali ya Tanganyika, Zanzibar na serikali ya Jamhuri.

Akizungumza katika kizindua rasimu ya katiba mpya iliyotokana na maoni ya wananchi mjini Dar es Salaam mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Joseph Warioba amesema licha ya wananchi kupendekeza mfumo wa maktaba, serikali nne, mbili, lakini tume imeshawishika na mfumo wa serikali tatu kufuatia maoni hayo.

Warioba amesema tume hiyo haijashawishika na maoni yaliotolewa na wananchi ya kuvunjwa kwa muungano

Amesema katika mfumo huo bunge la muungano litakuwa na wajumbe 75, 20 kutoka Zanzibar, 50 kutoka Tanganyika na watano watakaoteuliwa na rais kutoka kundi la watu wenye ulemavu.

Aidha warioba amesema katika rasimu hiyo tume imependekeza kuwepo wagombea binafsi na vyama vya siasa katika uchaguzi wa urais, ubunge, udiwani na wenyeviti wa vijiji.

Kuhusu ushindi wa kura wa nafasi ya urais tume hiyo imependekeza mgombea wa nafasi hiyo apate zaidi ya asilimia 50 ya kura badala ya mfumo wa sasa wa kura nyingi za mgombea.

Hata hivyo amesema matokeo hayo yanaweza kupingwa na chombo cha mahakama ya juu badala ya mfumo wa sasa wa tume ya uchaguzi ndio yenye mamlaka ya mwisho.

Zaidi ya watu Milioni moja na laki tano waliotoa maoni ya moja kwa maoja, kwa maandishi yakiwemo makundi 160 na maoni ya viongozi wa kitaifa na wastaafu.

Rasimu hiyo ya katiba inatarajiwa kusambazwa kwa wananchi ili kutoa nafasi kwa wajumbe wa baraza ya katiba kuisoma mapema kabla ya kuipitia kwenye mabaraza yao.

Advertisements