jumbeRais Mstaafu awamu ya pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Alhajj Aboud Jumbe Mwinyi leo ametimiza umri miaka 93 ya kuzaliwa.

Alhajj Jumbe amesema anamshukuru mwenyezi Mungu kwa  umri aliyomjaalia  kutokana na kushuhudia neema nyingi.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Ustadh Mohammed Yoyota katika hafla ya kumombea dua huko Kiembesamaki amesema Mwewnyezi Mungu amejalia huruma na hisani alipokabidhiwa dhamana ya kuongoza Zanzibar.

Hata hivyo amesema mwenyezi mungu alimuongoza pale alipoteleza na kumuomba kuitakasa amali yake pamoja na waislamu wenzake ili kuwa na majibu sahihi mbele yake.

Akitowa shukurani kwa waalikwa waliohudhuria dua hiyo mmoja wa mototo wake, Mustafa Aboud Jumbe amesema dua hiyo inatokana na utaratibu wa baba yao kusomewa.

Amesema familia hiyo inapata masuala mengi kuhusu hali ya  baba yao, lakini  amesema hajambo anazungumza na tatizo linalomsumbua ni uzee, nuru ya macho na usikivu.

Rais huyo mstaafu hajaonekana hadharani kwa miaka mingi sasa na anaishi nyumbani kweke Kigamboni mkoani  Dar es Salaam

Advertisements