Serikali imeombwa kuchukua hatua za haraka kupambana na vitendo vya uharamia vinavyoweza kuitia doa Zanzibar katika uhusiano wa kimataifa.

Akizungumza na Zenji fm radio mkurugenzi mipango wa AFP Rashid Mchenga amesema Zanzibar inahitajia uhusiano huo hivyo tukio la jana la kumwagiwa tindikali raia wawili wa Ungereza linaweza kupoteza sifa hiyo.

Amesema Zanzibar inaendelea na sera ya utalii kwa wote inayohitaji amani na autulivu kwa wageni na matukio kama hayo iwapo yataendelea yataathiri sekta ya utalii inayotegemewa kuimarisha uchumi.

Hivyo Mchenga amelitaka jeshi la polisi kuchukua hatua za haraka za upelelezi ili kuwabaini watu waliofanya kitendo hicho kwa kuwafikisha mahakamani….)

Nae mwakilishi wa mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu amelaani kitendo hicho na kusema kinachafua amani ya Zanzibar.

Amesema tukio hilo linatishia uchumi wa Zanzibar kupitia sekta ya utalii, hivyo amelitaka jeshi la polisi na mamlaka nyengine kufanya uchunguzi wa kina kuwajua waliohusika ili kuwafikisha mhakamani

Advertisements