Mji Mkongwe wa Zanzibar

Mji Mkongwe wa Zanzibar

Raia wawili wa Uingereza waliomwagiwa tindikali jana maeneo ya Mji Mkongwe wanatarajiwa kusafirishwa leo kuelekea nchini kwao Uingereza kwa ajili ya matibabu zaidi.

Akizungumza na Zenji fm radio kamanda wa polisi wa mkoa wa mjini Magharib Mkadam Khamis Mkadam amesema awali raia hao wenye umri wa miaka 18 mara baada ya tukio hilo walisafirishwa mjini Dar es Salaam.

Mkadam amesema jeshi la polisi linaendelea na upelelezi kuwasaka watu waliohusika na tukio hilo.

Kate Gee na Kirstie Trup ni wafanyakazi wa shirika moja ya kujitolea walikuwa wakisomesha skuli ya Tomondo walimwagiwa tindikali sehemu za mikononi, uso na kifua na watu wawili waliokuwa kwenye vespa jana usiku.

Hii ni mara ya kwanza kwa raia wa kigeni kushambiliwa kwa kumwagiwa tindikali.

Advertisements