Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka akisisitiza kitu alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Gymkana Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar)

Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka akisisitiza kitu alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Gymkana Mjini Zanzibar.
(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar)

Jumuiya ya UVCCM  imemtaka  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein kumfukuza kazi Mwanasheria Mkuu wa Serikali   ya Mapinduzi Zanzibar Othman Masoud Othman kufuatia matamshi yake  yanayokinzana na kupingana na dhamana aliyopeewa na Rais aliyemteua.

     Msimamo huo umetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika Afisi Kuu ya Jumuiya hiyo huko Gymkhana mjini Unguja.

Shaka amesema matamshi ya kutaka muundo wa Muungano wa Seriikali tatu yamesigana na dhamana pamoja na kukiuka amana ya kimajukumu ya kikatibab aliyopewa ya  kusimamia na kuitetea ipasavyo Serikali ya Zanzibar.

Amesema kitendo cha kushiriki kongamano na kujitambulisha kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali huku akiweka  msimamo  na kupendekeza  muundo wa Serikali tatu badala ya mbili kwa  Serikali anayoitumikia kama mtumishi  wa SMZ  ni kukiuka maadili ya ajira yake .

UVCCM imesema kama kweli Othman ni muungwana, anayeheshimu utetezi na msimamo wake wa kushabikia muundo wa Serikali tatu aonyeshe ujasiri na kujiondoa Serikalini mara moja.

Aidha Naibu huyo Katibu Mkuu wa UVCCM amesema ni kuinyume na taratibu kwa msaidizi wa Rais upande wa masuala ya sheria aliyeapa kumsaidia, kulinda katiba ya Zanzibar, kuitetea na kuihifadhi akipita njia tofauti ya kisera na Rais wake.

Shaka amesema ni vyema  Othman akaipinga SMZ akiwa nje kwani  kubaki  ndani ya chombo hicho kazi yake si kupinga bali ni kushauri au kusema baada ya kushauriana na Rais.

Alisema ipo haja kwa Rais  Dk Shein kumfukuza kazi Mwanasheria Mkuu huyo  kwa kitendo chenye bashara ya usaliti na kubeza matakwa ya kisera ya Rais aliyemteua na kumpa dhamana alionayo.

Hata hivyo Naibu huyo Katibu mkuu alipoulizwa ikiwa Rais na Mwanasheria Mkuu  watakataa kutimiza dai  lao ,amesema jumuiya yake itafanya  maandamano ya amani ya kumshinikiza Rais amuondoe Mwanasheria Mkuu huyo Serikalini.

Mwanasheria Mkuu wa SMZ Othman Masoud Othman alipopigiwa siku ili atoe maoni na msimamo wake amesema yuko kwenye Ndege akisafiri kuelekea Doha, nchini Qatar na atajibu hayo atakapokuwa katika nafasi nzuri.

Advertisements