Archive for September, 2013

BALOZI ZA TANZANIA ZATAKIWA KUTANGAZA SERA ZA UCHUMI

DRRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema ofisi za kibalozi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchi za nje hazinabudi kuendelea kuzitangaza vyema sera za uchumi na uwekezaji za Tanzania ili iendelee kufanya vizuri zaidi katika kuimarisha sekta hizo.

Amesema uchumi wa Tanzania umeonekana kukua vizuri kutokana na mchango mkubwa unaotokana na sekta ya uwekezaji na utalii, hivyo ni vyema mkazo maalum ukawekwa katika kuimarisha sekta hizo nchi za nje.

Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati alipokuwa akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Ethiopia Bibi Naimi Azizi ambaye alifika Ikulu Zanzibar kumuaga.

Rais wa Zanzibar amesema ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia imeanza kufanya kazi miaka mingi iliyopita jambo ambalo siyo tu linatoa fursa ya kipekee katika kufanya shughuli zake kwa ufanisi, lakini hatua hiyo itasaidia pia kuitangaza Tanzania kiutalii na kiuwekezaji katika nchi mbali mbali duniani.

Amefafanua kuwa ingawa sekta hizo zimekuwa zikifanya vizuri, bado fursa ipo ya kuweza kufanya vizuri zaidi, iwapo juhudi za makusudi zitachukuliwa kuzitangaza nchi za nje.

Akizungumzia mfano wa Ethiopia, amesema nchi hiyo kupitia shirika lake la ndege la “Ethiopian Airlines”, linalofanya safari za moja kwa moja nchini Tanzania, linaweza kuwa kichocheo kikubwa katika kukuza biashara ya utalii nchini.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ameongeza kuwa, Zanzibar bado inahitaji kupokea watalii wengi zaidi ili kufikia lengo ililojiwekea la watalii 500,000 kwa mwaka ifikapo mwaka 2015. Hadi sasa inapokea watalii 200,000 kwa mwaka.

Akizungumzia maendeleo ya lugha ya Kiswahili, Rais wa Zanzibar amemuomba Balozi huyo kusisitiza haja ya kuzungumza lugha ya Kiswahili kila fursa ya kufanya hivyo inapopatikana, kwani alisema licha ya Umoja wa Afrika kukubali kuitumia lugha hiyo, bado matumizi yake hayajafikia kiwango kinachohitajika hasa katika medani za kimataifa.

Naye Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ethiopia Bibi Naimi Azizi ameahidi kuwa atafanya kila linalowezekana kuhakikisha anatekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa maslahi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiuchumi na kijamii.

Advertisements

MAHAKAMA YASHINDWA KUANDIKA HUKUMU DHIDI YA VIONGOZI WA UAMSHO

DDDKesi inayowakabili viongozi wa jumuiya ya Uamsho imeakhirishwa hadi Octoba 1 mwaka huu kutokana na kutokamilika uandikaji wa hukumu wa kesi hiyo.

Mwendesha mashitaka wa serikali Ramadhani Abdalla amesema kesi huyo imefikishwa mbele ya mahakama hiyo kwa kutolewa mamuzi ya kuwa watuhumuwa wana kesi ya kujibu au hawana.
Watuhumiwa hao ni Musa Juma Isa,faridi Hadi Ahmedi, Haji Sadifa Haji, Sleiman Juma Sleima, Fikirini majaliwa Fikirini na Abdalla Said Ali wotw kwa pamoja wanakabiliwa na  tuhuma za kufanya mhadhara wa kislamu bila ya kibali cha Mufti.
Wote kwa pamoja mnamo Juni 26 ,2012 wakati wa saa  3.00 Asubuhi huko Lumumba walifanya mhadhara wa kislamu bila kuwa na kibali cha Mufti
Kitendo ambacho ni kinyume na kifungu  cha 6(1) (4) cha kanuni ya kuidhinisha na kudhibiti mihadhara chini ya kifungu cha 15 (1) cha sheria namba ya mwaka 2001.
Hakimu wa mahkama ya wilaya anaesikiliza kesi hiyo Msaraka Pinja ameikhirisha kesi hiyo hadi Octoba 1 na watuhumiwa walirudi rumande

NITAKAZA MKWIJI BAADA YA WAHISANI KUPUNGUZA MISAADA YA UKIMWI-DR. SHEIN

SHINRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema jitihada za kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya ugonjwa wa UKIMWI nchini hazina budi ziende sambamba na vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vingine ambavyo ni miongoni mwa vyanzo vya ugonjwa huo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Kituo cha Jamii na Watoto huko Welezo Wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo Dk. Shein amesema imebainika kuwa maambukizi mapya ya virusi vya ugonjwa huo kwa vijana yanahusishwa na matumzi ya madawa ya kulevya.

“Katika miaka ya hivi karibuni imebainika kuwa maambukizi mapya ya UKIMWI yanawakumba zaidi vijana wanaotumia dawa za kulevya hapa nchini” Dk. Shein alieleza.

Kituo hicho kimejengwa na Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ugonjwa wa UKIMWI Zanzibar ZAPHA+ kwa msaada wa taasisi ya Stephen Lewis Foundation ya Canada ambayo ilichangia shilingi milioni 43.65 ambazo ni sawa na asilimia 40.45

Kwa hivyo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali na washirika wengine katika mapambano dhidi ya maambukizi ya UKIMWI na dawa za kulevya kuiokoa jamii hasa vijana ambao ni tegemeo la taifa.

Dk. Shein amewaeleza wanachama wa ZAPHA+, wananchi na wageni waliohudhuria hafla hiyo kuwa tangu ugonjwa huo ulipogunduliwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikifanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuhakikisha Zanzibar haipati maambukizi mapya na pia kuondosha unyanyapaa dhidi ya watu walioathirika na ugonjwa huo.

“…Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikichukua hatua mbali mbali ili kuhakikisha kwamba tunakuwa na Zanzibar isiyokuwa na maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI, isiyokuwa na unyanyapaa wala ubaguzi unaotokana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI” Dk. Shein alieleza.

Amezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kuunda taasisi za kuratibu na kushughulikia mapambano dhidi ya ugonjwa huo, kushiriki katika kutekeleza sera, mipango, na mikakati mbalimbali kwa kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika mapambano hayo.

Kwa hiyo ametoa wito kwa wananchi kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya UKIMWI kwa kuzingatia utekelezaji wa mipango iliwekwa na Serikali kwa kushirikiana na sekta zisizokuwa za Serikali.

Kuhusu huduma na tiba kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ameeleza kuwa zimeendelea kuimarishwa kwa kuongeza vituo vya huduma na tiba hadi kufikia vituo kumi kutoka kituo kimoja mwaka 2005.

“…dawa za ARV zimekuwa zikipatikana katika vituo mbalimbali bila malipo…huku serikali imeimarisha huduma za uchunguzi wa maradhi ili kuongeza ufanisi katika kukabiliana na janga hili” Dk. Shein alibainisha.

Dk. Shein ameupongeza uongozi wa ZAPHA+ na wanachama wake kwa jitihada zao hadi kuweza kujenga jengo hilo ambalo litawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Akizungumzia kuendelea kupungua kwa misaada ya wafadhili kwa shughuli za UKIMWI Dk. Shein ameahidi kuwa Serikali itaendelea kutafuta namna bora ya kusaidiana na taasisi kama ZAPHA+ ili kutekeleza majukumu ya mapambano dhidi ya UKIMWI.

Hata hivyo ametoa wito kwa uongozi wa ZAPHA+ kutafuta njia za kujiongezea mapato kwa kubuni miradi ikiwemo ya kujitegemea.

Amewataka wananchi kutumia fursa ya kuwepo kwa jumuiya hiyo kwa kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu maradhi ya UKIMWI kwa manufaa yao binafsi na pia kama sehemu ya jitihada za pamoja kupambana na maradhi hayo nchini.

Rais alitumia fursa hiyo kuwashukuru watu na taasisi mbali mbali ambazo zimekuwa zikisaidia Zanzibar katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI tangu kugundulika kwake hapa Zanzibar miaka 27 iliyopita.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna, Waziri wa Afya Juma Duni Haji,Mkuu wa Mkoa Mjini Maghribi Abdalla Mwinyi Khamis na washirika mbalimbali wanaounga mkono mapambano dhidi ya UKIMWI yakiwemo Mashirika ya Kimataifa

KINDUMBWE NDUMBWE CHA KATIBA MPYA-CUF

DDDChama cha wananchi CUF kinakusudia kuzuwia wabunge wake na wale wanaokiunga mkono chama hicho kushiriki katika bunge la katiba iwapo muswada wa sheria wa mabadiliko ya katiba uliopitishwa na bunge hivi karibuni utatiwa saini na rais.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara Kibandamaiti katibu mkuu wa CUF Malim Seif Sharif Hamad amesema mswada huo unahitaji kupata maoni ya serikali ya Mapinduzi Zanzbzibar na jumuiya za kiraia.

Amasema iwapo rais Kikwete atatia saini atawazuwi wabunge wa CUF na wanaounga mkono chama hicho kuhudhuria bunge la katiba litakalopitisha rasimu ya mwisho ya katiba kabla ya kupigiwa kura ya maoni na wananchi kuwa katiba kamili.

Aidha Maalim Seif ameyataja baadhi ya vipengele vinavyodaiwa na CUF havikubaliani navyo ni kupitishwa kwa rasimu ya katiba kwa wingi wa kura za wajumbe badala ya thuluthi mbili ya kila upande.

Amesema katika mswada huo serikali ilitoa mapendekezo ya awali sita, lakini baada ya kuwasilishwa kulifanyika marekebisho mengine ya vipengele vinane bila ya kuarifiwa upande wa Zanzibar.

Amesema kamati ya bunge ya katiba na sheria pia ilitakiwa kuja Zanzibar kupata maoni ya jumuiya za kiraia, lakini haikufanya hivyo na badala yake kuchukua maoni ya jumuia za Tanzania bara pekee.

Muswada huo wa sheria ulipitishwa na bunge hivi karibuni pia umesusiwa na vyama cha CHADEMA na NCCR-MAGEUZI vilivyounda muungano na kukishirikisha chama cha CUF kuwa na sauti moja ya kuupinga.

MGAO WA UMEME TENA ZANZIBAR

MRADIWananchi wa kisiwa cha Unguja watarejea tena katika magao wa huduma ya umeme baada ya kubainika matatizo ya kiufundi ya waya mpya wa umeme wa megawati 100 kutoka Tanzania bara.

Akitoa taarifa kwa wananchi juu ya mgao huo waziri wa ardhi, makaazi, maji na nishati Ramadhan Abdalla Shaaban amesema katika kipindi cha marekebisho italazimika kutumia waya wa zamani wa Megawati 45 utakaotoa umeme wa mgao.

Amesema mgao huo utakaodumu kwa siku 24 utanza tarehe 25 mwezi huu hadi Octoba 10 wakati wa kipindi cha matumizi makubwa ya umeme kwa wananchi kuanzia saa 12.00 jioni hadi saa 5.00 usiku)

Amesema hatua hiyo inataokana na wakandari kufanya uchaunguzi wa kina na kubaini baadhi ya mashimo ya kusimamishia nguzo hayakufikiwa viwango vya uimara kwa mujibu wa vigezo vya kiufundi.

Ameyataja mashimbo hayo ambayo manne yako Tanzania bara na moja liko Unguja yatafanyiwa marekebisho na mkandarasi kwa kutumia gharama zake mwenyewe.

Waya mpya wa umeme wa Megawati 100 unaoleta uemem kutoka Tanzania bara uliogharamiwa na serikali ya Marekani ulizinduliwa April mwaka huu ili kumaliza tatizo la mgao wa umeme uliosababisha na kuchakaa kwa waya wa zamani wa megawati 45.

Shambulio la Nairobi lauwa watu kadha

BREAKWatu waliokuwa na silaha wamefyatua risasi mjini Nairobi, Kenya, kwenye eneo la maduka katika mtaa wa Westlands.

Walioshuhudia tukio hilo, wanasema kuwa maguruneti piya yalitumika.

Inaarifiwa watu watano wamekufa.

Mwandishi wetu mjini Nairobi anaeleza kuwa washambuliaji inaarifiwa walivaa vilemba kama vya al-Shabaab, lakini haikuthibitishwa kama wapiganaji hao wamehusika.

Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira jengo la maduka liitwalo Westgate, katika mtaa wa Westlands, na kuna taarifa ya watu waliojeruhiwa wakitolewa hapo kwa machera.

Inaarifiwa kuwa watu wengi wamenasa ndani ya jengo.

Magari yaliyoegeshwa nje ya maduka yameharibika

 

WALIOMUUWA PADRI WATAKIONA-DR. SHEIN

padri-mlandegeRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa wito kwa Jeshi la Polisi nchini kujitahidi kuimarisha uchunguzi wa  matukio ya watu kumwagiwa tindikali ili wahusika wapelekwe kwenye vyombo vya sheria.

 

Dk. Shein ametoa wito huo leo huko hospitali la Mnazi Mmoja mjini Unguja alipokwenda kumjulia hali Padri Anselmo Mwang’amba wa Kanisa Katoliki, Machui Unguja, ambae amelazwa katika hospitali hiyo kufuatia kumwagiwa tindikali jana jioni.

 

“hatuwezi kuviacha vitendo hivi viendelee… ni lazima Jeshi la Polisi lijitahidi kuwatafuta wahusika ili sheria ichukue mkondo wake” alisisitiza Dk. Shein.

 

Amekieleza kitendo hicho kuwa ni cha kikatili na kisichovumika na kuongeza kuwa wahusika lazima wasakwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

 

Dk. Shein amesema amesikitishwa na kitendo hicho na kumpa pole Padri Mwang’amba na kumuomba Mwenzi Mungu ampe nafuu haraka apone ili endelee kuitumikia jamii.

 

Akizungumza na waumini wa kanisa hilo nje ya Wodi alipolazwa Padri huyo Dk. Shein aliwataka waumini hao kuwa na subira wakati Serikali ikichukua hatua kukabiliana na kitendo hicho.

 

“Ni jambo la kusikitisha kumfikisha binadamu wenzako katika hali kama hii ya majonzi. Hakuna anayeyataka haya. Tuwe wastahamilivu Serikali tunachukua hatua”aliwaambia waumini hao.

 

Akizungumzia hali yake, Padri Mwang’mba alimueleza Rais kuwa hali yake ni nzuri na anaona vizuri lakini anatarajia kupata nafuu zaidi baada ya uvimbe kupungua sehemu za machoni.

 

“Hali yangu ni nzuri lakini natarajia uvimbe ukipungua nitaona vizuri zaidi” alisema Padri Mwang’amba na kuongeza kuwa ilikuwa ni bahati kwake hakuathirika sana.

 

Amefafanua kuwa tukio hilo lilitokea eneo la Mlandege jioni wakati akitoka katika ofisi moja inayotoa huduma za intaneti/mtandao katika eneo hilo ndipo akatokea kijana mmoja na kumwagia tindikali.

 

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk. Mohamed Saleh Jidawi akiwa amefuatana na Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dk. Jamala Adam Taibu amesema alipofikishwa katika hospitali hiyo Padri Mwang’amba alipatiwa huduma zote muhimu za matibabu zinazostahiki.

 

Kuhusu majeraha aliyopata Dk. Jidawi alieleza kuwa kwa ujumla asilimia 30 ya mwili wa Padri Mwang’amba umeathirika na kidogo sehemu za macho.