DDDChama cha wananchi CUF kinakusudia kuzuwia wabunge wake na wale wanaokiunga mkono chama hicho kushiriki katika bunge la katiba iwapo muswada wa sheria wa mabadiliko ya katiba uliopitishwa na bunge hivi karibuni utatiwa saini na rais.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara Kibandamaiti katibu mkuu wa CUF Malim Seif Sharif Hamad amesema mswada huo unahitaji kupata maoni ya serikali ya Mapinduzi Zanzbzibar na jumuiya za kiraia.

Amasema iwapo rais Kikwete atatia saini atawazuwi wabunge wa CUF na wanaounga mkono chama hicho kuhudhuria bunge la katiba litakalopitisha rasimu ya mwisho ya katiba kabla ya kupigiwa kura ya maoni na wananchi kuwa katiba kamili.

Aidha Maalim Seif ameyataja baadhi ya vipengele vinavyodaiwa na CUF havikubaliani navyo ni kupitishwa kwa rasimu ya katiba kwa wingi wa kura za wajumbe badala ya thuluthi mbili ya kila upande.

Amesema katika mswada huo serikali ilitoa mapendekezo ya awali sita, lakini baada ya kuwasilishwa kulifanyika marekebisho mengine ya vipengele vinane bila ya kuarifiwa upande wa Zanzibar.

Amesema kamati ya bunge ya katiba na sheria pia ilitakiwa kuja Zanzibar kupata maoni ya jumuiya za kiraia, lakini haikufanya hivyo na badala yake kuchukua maoni ya jumuia za Tanzania bara pekee.

Muswada huo wa sheria ulipitishwa na bunge hivi karibuni pia umesusiwa na vyama cha CHADEMA na NCCR-MAGEUZI vilivyounda muungano na kukishirikisha chama cha CUF kuwa na sauti moja ya kuupinga.

Advertisements