Archive for October, 2013

MGAO WA ASILIMIA 4.5 BAS-MALIM SEIF

Malim Seif Sharif Hamad

Malim Seif Sharif Hamad

Makamu wa kwanza rais Zanzibar Malim Seif Sharif Hamad amesema asilimia 4.5 ya gawio la Zanzibar litokanalo na misaada ya kimataifa na faida ya benki kuu Tanzania BOT ni ndogo. Akizungunza na wandishi wa habari juu ya mafanikio ya miaka mitatu ya serikali ya umoja wa kitaifa huko hoteli ya Ocean View amesema mgao huo unahitaji kurekebishwa hadi kufikia asilimia 11.3. Malim Seif amesema asilimia hiyo ya fedha za Zanzibar ndizo zilizotumika kuanzishia mtaji wa BOT kufuatia bodi ya Sarafu ya Afrika ya Mashariki kuvunjika mwaka 1963. …Hata hivyo amesema mazungumzo ya kurekebisha gawio hilo yanaendelea kupitia ngazi za viongozi wakuu wa serikali ya muungano na Mapinduzi Zanzibar. Akizungumzia mafanikio ya miaka mitatu ya serikali ya umoja wa kitaifa Malim Seif amesesema Zanzibar bado inakabiliwa na upungufu wa madaktari na kutoa huduma za afya zisizowaridhisha wananchi. Hata hivyo amesema serikali imechukua juhudi za kuwafundisha vijana 34 katika chuo cha udaktari Zanzibar wanaotarajiwa kumaliza mwakani.

Advertisements

KAMPUNI ZA MAFUTA KUZUNGUMZA NA ZANZIBAR

Kampuni za uchimbaji wa mafuta zilizopewa mikataba ya utafutaji na uchimbaji wa nishati hiyo na serikali ya muungano zimeanza kuwasiliana na Zanzibar baada ya suala hilo kutaka kuondolewa kwenye muungano.

Waziri wa ardh, makaazi, maji na nishati Ramadhan Abdalla Shaaban amesema hatua hiyo inatokana na wajumbe wa baraza la wawakilishi kutaka mafuta na gesi kuondolewa kwenye oroha ya mambo ya muungano

Akizungumza katika semina ya wajumbe wa baraza la wawakilishi juu ya uwezekano wa Zanzibar kuwepo mafuta na gesi amsesema kampuni za Rak Gas na Shell zimeanza kuwasiliana na serikali ya Mapinduzi kufufua maeneo waliopewa na serikali ya muungano

Nayo kampuni ya Rak Gas kutoka Rass-helma imetahadharisha juu ya ucheleweshaji wa uchimbaji wa mafuta na gesi Zanzibar unaweza kukosesha soko la kuzia nishati hiyo.

Mkuu wa uendeshaji wa kampuni ya Rak gas Joseph Haskel amesema nchi jirani za Kenya na Uganda ambazo zimo katika hatua ya mwisho ya uchimbaji wa mafuta zinaweza kuhodhi soko la Zanzibar.

Akiwasilisha mada katika semina ya wajumbe wa baraza la wawakilishi juu ya kuwepo dalili za mafuta na gesi amesema utafiti wa mwaka 1982 Zanzibar umegundua kuwepo dalili za mafuta maeneo ya juu na gesi maeneo ya baharini

SMZ KUPITIA SHERIA YA VILEO YA 1928

CCSerikali ya mapinduzi Zanzibar inafanya mapitio ya sheria ya vileo ya mwaka 1928 ili kuweka utaratibu utakaozuwia uanzishwaji wa baa na vilabu vya pombe katika maeneo ya makaazi ya wananchi.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi waziri wa nchi ofisi ya rais, tawala za mikoa na vikosi maalum Haji Omar Kheir amesema serikali kwa kuzingatia utamaduni wa watu utowaji wa leseni za kuendeshea biashara hiyo unazingatiwa kwa umakini.

Aidha amesema serikali imeanzisha mahakama ya vileo kuwawezesha wananchi kutoa pingamizi za kuzuwia leseni za biashara hiyo endapo wataona zitaharibu mila na utamadun..

Waziri Kheir amesema uanzishwaji wa vilabu vya pombe au baa unaweza kusababisha kuporomoka maadili na hatimae kuathirika mila na utamaduni kwa vijana.

Serikali ya Mapinuzi Zanzibar bado inatumia sheria ya mwaka 1928 iliyotungwa na wakoloni kuendeshea biashara ya vileo inayonekana kupitwa na wakati.

WANANCHI WAHIMIZWA KUHIFADHI MILA NA UTAMADUNI WAO

 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na Naibu Kadhi Mkuu Sheikh Hassan Othman Nwali (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Pemba Juma Khamis wakimsalia Mtume katika hafla ya Maulid yaliyofanyika Tumbatu Jongowe. (Picha na Salmin Said, OMKR).

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na Naibu Kadhi Mkuu Sheikh Hassan Othman Nwali (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Pemba Juma Khamis wakimsalia Mtume katika hafla ya Maulid yaliyofanyika Tumbatu Jongowe. (Picha na Salmin Said, OMKR).

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amewahimiza wananchi wa Zanzibar kuungana katika kulinda na kuhifadhi utamaduni, mila na silka za Wazanzibar, ili kuepusha tabia ya kuipotosha kwa makuasudi inayofanywa na baadhi ya watu.  

Maalim Seif ameyasema hay oleo, wakati alipokuwa akihutubia katika hafla ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), yaliyoandaliwa na Madrasat Nur Islamiya huko katika kijiji cha Tumbatu Jongowe, Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja.
Amesema utamaduni na mila za Wazanzibari ni za kipekee na vuimerithiwa kwa miaka mingi, lakini baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kuvipotosha kwa malengo maalum, jambo ambalo linapaswa kupigwa vita na wananchi kulikataa.
Amesema historia ya Zanzibar ina mafungamano makubwa na Dini ya Kiislamu kwa zaidi ya miaka 1000, hali ambayo inathibitishwa na kuwepo maeneo mengi ya kihistoria, ikiwemo msikiti wa Kizimkazi, magofu ya majengo ya asili huko Makutano katika kisiwa cha Tumbatu, pamoja na athari za iliyopo katika eneo la Kihistoria la Mkuu, kisiwani Pemba.
Aidha, Makamu wa Kwanza wa Rais amesema malengo hayo yataweza kufikiwa iwapo Walimu, Masheikh na Wazee watakuwa na tabia ya kuwafunza watoto wao historian a utamaduni wa nchi yao.
Makamu wa Kwanza wa Rais pia ametumia hafla hiyo kuhimiza umoja na mshikamano miongoni mwa Wazanzibari wote hasa wakati huu wa kutafuta Katiba mpya ya Tanzania, ili kuweza kulinda maslahi na musatakabala mwema wa Zanzibar.
“Tukishikamana tutakuwa wamoja, tutaweza kutetea na kulinda maslahi ya nchi na watu wake, tukigawana na kuweka mbele maslahi binafsi, badala ya kuweka mbele maslahi ya Taifa tutashindwa kuitumia vyema fursa hii”, alisema Maalim Seif.
Katika risala yao wana Madrasa hao wa Nur Islamiya waliwapongeza wananchi na viongozi mbali mbali, kutokana na michango yao iliyowezesha Madrasa hiyo kujengwa katika kipindi kifupi.
Katika risala hiyo iliyosmwa na Maalim Juma Makame, waliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali, pamoja na wananchi wa kijiji hicho katika kuwajenga watoto katika maadili mema, ili wawe wananchi wema wanaoweza kutegewa na Taifa.   
Nae, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Hassan Othman Ngwali akihutubia katika hafla hiyo, amewahimiza waumini wa Kiislamu kuzidisha bidii katika kumsifu Mtume Muhammad (S.A.W), na kushikamana na mafundisho yake kivitendo.
Maulid hayo ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) hufanyika kila mwaka ifikapo mwezi 12 Mfunguo tatu.   

NYUMBA YA BIKIDUDE KUGEUZWA KUMBUKUMBU YA TAIFA?

H

Hii ndio nyumba ya bikidude iliyopo mtaa wa Rahaleo

Wizara ya habari, utamaduni, utalii na michezo imesema wazo la kuifanya nyumba ya msanii maarufu Zanzibar marehemu Kidude binti Baraka kuwa makumbusho ya taifa itategemea ruhusa ya warithi wake.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi naibu waziri Bihindi Hamad Khamis amesema wazo hilo linahitaji likubaliwe na warithi wa marehemu ambao ndio wamiliki wa nyumba hiyo na sio serikali.

Amesema serikali inachokifanya ni kukusanya kazi za msanii huyo na kuzihifadhi kwenye maktaba na kuzitumia kwenye maadhimisho ya kuwaenzi wasanii marufu wa Zanzibar yanayofanyika kila mwaka.

Bi Kidude aliefariki April mwaka huu, sanaa zake za nyimbo na mambo ya utamaduni ni kivutio kwa wananchi, watalii na watafiti wa mambo ya muziki.

SIASA CHAFU ZANZIBAR ZINAWEZA KULETA MAAFA-ABOUD

Mohammed Aboud Mohammed

Mohammed Aboud Mohammed

Waziri wa nchi ofisi wa makamu wa pili wa rais Mohammed Aboud ameonya juu kujichomoza siasa chafu Zanzibar zinazoweza kusababisha maafa kwa wananchi.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku maafa duniani yalifanyika hoteli ya Bwawani amesema siasa zinazolenga kugombanisha watu, kuchukiana zinaweza kuitumbukiza nchi katika majanga.

Amesema vitendo vya kumwagiwa tindikali ni miongoni mwa silaha za maangamizi duniani, vinahitaji kuzungumzwa bila ya kuoneana haya kwa vile vinasabadisha maafa.

Abodua amesema licha ya juhudi zinazofanyika za kuepukana na tofauti za kisiasa Zanzibar, lakini wengine wanatafuta mbinu mpya za kuleta mitafaruki.

Nao washiriki wa mkutano huo kutoka jumuiya za kiraia na taasisi za serikali wamesema Zanzibar bado haijachukua juhudi za kuimarisha shughuli za ukozi licha ya kukumbwa na majanga ya kuzama kwa meli.

Zanzibar ilikumbwa na maafa yaliosababisha watu wengi kufariki dunia likiwemo janga la ugonjwa wa kipindupindi mwaka 1978, ajali ya meli ya Mv Spice Islander 2011 na Mv. Skygit mwaka jana

ABOUBAKAR ATOFAUTIANA NA BOSI WAKE

Waziri wa sheria na katiba Zanibar Aboubakar Khamis Bakary

Waziri wa sheria na katiba Zanibar Aboubakar Khamis Bakary

Wizara ya sheria na katiba Zanzibar imesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar haikushirikishwa katika nyongeza ya vipengele 12 vya mswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba mpya ya Tanzania.

Kauli hiyo ya waziri Abubakar Khamis Bakar iliyotolewa leo baraza la wawakilishi inapingana na ile iliyotolewa na Makamu wa pili wa rais balozi Seif Ali Iddi kusema serikali imeshirikishwa.

Akijibu suala katika kikao cha baraza hilo amesema serikali ilishirikishwa hatua ya awali ya mswada huo uliokuwa na vipengele vinne, lakini baada ya kuongezwa vipengele vingine 12 serikali haikushirikishwa..

Hivi karibuni makamu wa pili wa rais balozi Seif Ali Iddi amesema kauli yake ilyotowa bungeni wakati wa kupitishwa mswada huo ya kushirikishwa kwa Zanzibar ilikuwa sahihi na hajakurupuka