FUNGU MBARAKMwakilishi wa jimbo la Uzini Mohammed Raza ameiomba serikali kufanya tathimini ya visiwa vidogo baada ya kuwepo taarifa za kutaka kuchukuliwa kisiwa cha Fungu Mbaraka.

Akichangia mswaada wa sheria wa mabadiliko ya ardhi katika kikao cha baraza la wawakilishi amesema kumekuwepo na taarifa za kisiwa hicho kudaiwa kimo ndani ya mipaka ya Tanzania bara.

Raza amesema ni muhimu kwa serikali kuliweka bayana suala hilo  hasa kipindi hichi cha harakati za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ili kuviepusha vizazi vijavyo kuingia ndani ya mgogogo

Advertisements