H

Hii ndio nyumba ya bikidude iliyopo mtaa wa Rahaleo

Wizara ya habari, utamaduni, utalii na michezo imesema wazo la kuifanya nyumba ya msanii maarufu Zanzibar marehemu Kidude binti Baraka kuwa makumbusho ya taifa itategemea ruhusa ya warithi wake.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi naibu waziri Bihindi Hamad Khamis amesema wazo hilo linahitaji likubaliwe na warithi wa marehemu ambao ndio wamiliki wa nyumba hiyo na sio serikali.

Amesema serikali inachokifanya ni kukusanya kazi za msanii huyo na kuzihifadhi kwenye maktaba na kuzitumia kwenye maadhimisho ya kuwaenzi wasanii marufu wa Zanzibar yanayofanyika kila mwaka.

Bi Kidude aliefariki April mwaka huu, sanaa zake za nyimbo na mambo ya utamaduni ni kivutio kwa wananchi, watalii na watafiti wa mambo ya muziki.

Advertisements