Kampuni za uchimbaji wa mafuta zilizopewa mikataba ya utafutaji na uchimbaji wa nishati hiyo na serikali ya muungano zimeanza kuwasiliana na Zanzibar baada ya suala hilo kutaka kuondolewa kwenye muungano.

Waziri wa ardh, makaazi, maji na nishati Ramadhan Abdalla Shaaban amesema hatua hiyo inatokana na wajumbe wa baraza la wawakilishi kutaka mafuta na gesi kuondolewa kwenye oroha ya mambo ya muungano

Akizungumza katika semina ya wajumbe wa baraza la wawakilishi juu ya uwezekano wa Zanzibar kuwepo mafuta na gesi amsesema kampuni za Rak Gas na Shell zimeanza kuwasiliana na serikali ya Mapinduzi kufufua maeneo waliopewa na serikali ya muungano

Nayo kampuni ya Rak Gas kutoka Rass-helma imetahadharisha juu ya ucheleweshaji wa uchimbaji wa mafuta na gesi Zanzibar unaweza kukosesha soko la kuzia nishati hiyo.

Mkuu wa uendeshaji wa kampuni ya Rak gas Joseph Haskel amesema nchi jirani za Kenya na Uganda ambazo zimo katika hatua ya mwisho ya uchimbaji wa mafuta zinaweza kuhodhi soko la Zanzibar.

Akiwasilisha mada katika semina ya wajumbe wa baraza la wawakilishi juu ya kuwepo dalili za mafuta na gesi amesema utafiti wa mwaka 1982 Zanzibar umegundua kuwepo dalili za mafuta maeneo ya juu na gesi maeneo ya baharini

Advertisements