CCSerikali ya mapinduzi Zanzibar inafanya mapitio ya sheria ya vileo ya mwaka 1928 ili kuweka utaratibu utakaozuwia uanzishwaji wa baa na vilabu vya pombe katika maeneo ya makaazi ya wananchi.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi waziri wa nchi ofisi ya rais, tawala za mikoa na vikosi maalum Haji Omar Kheir amesema serikali kwa kuzingatia utamaduni wa watu utowaji wa leseni za kuendeshea biashara hiyo unazingatiwa kwa umakini.

Aidha amesema serikali imeanzisha mahakama ya vileo kuwawezesha wananchi kutoa pingamizi za kuzuwia leseni za biashara hiyo endapo wataona zitaharibu mila na utamadun..

Waziri Kheir amesema uanzishwaji wa vilabu vya pombe au baa unaweza kusababisha kuporomoka maadili na hatimae kuathirika mila na utamaduni kwa vijana.

Serikali ya Mapinuzi Zanzibar bado inatumia sheria ya mwaka 1928 iliyotungwa na wakoloni kuendeshea biashara ya vileo inayonekana kupitwa na wakati.

Advertisements