Malim Seif Sharif Hamad

Malim Seif Sharif Hamad

Makamu wa kwanza rais Zanzibar Malim Seif Sharif Hamad amesema asilimia 4.5 ya gawio la Zanzibar litokanalo na misaada ya kimataifa na faida ya benki kuu Tanzania BOT ni ndogo. Akizungunza na wandishi wa habari juu ya mafanikio ya miaka mitatu ya serikali ya umoja wa kitaifa huko hoteli ya Ocean View amesema mgao huo unahitaji kurekebishwa hadi kufikia asilimia 11.3. Malim Seif amesema asilimia hiyo ya fedha za Zanzibar ndizo zilizotumika kuanzishia mtaji wa BOT kufuatia bodi ya Sarafu ya Afrika ya Mashariki kuvunjika mwaka 1963. …Hata hivyo amesema mazungumzo ya kurekebisha gawio hilo yanaendelea kupitia ngazi za viongozi wakuu wa serikali ya muungano na Mapinduzi Zanzibar. Akizungumzia mafanikio ya miaka mitatu ya serikali ya umoja wa kitaifa Malim Seif amesesema Zanzibar bado inakabiliwa na upungufu wa madaktari na kutoa huduma za afya zisizowaridhisha wananchi. Hata hivyo amesema serikali imechukua juhudi za kuwafundisha vijana 34 katika chuo cha udaktari Zanzibar wanaotarajiwa kumaliza mwakani.

Advertisements