Archive for November, 2013

MAITI AZAA MTOTO BAADA YA KUNYONGWA UTURUKI

UTURUKIKatika hali isiyo ya kawaida, watu wa mji wa Kaharisi nchini Uturuki wameshuhudia tukio la ajabu la kuzaliwa kitoto kichanga cha miezi saba baada ya mama yake kunyongwa. Kwa mujibu wa habari zilizotolewa, mtoto huyo wa kiume amezaliwa akiwa na afya nzuri. Habari zaidi zinasema kuwa, daktari wa gereza aliukimbilia mwili wa Sabah Mosilibasa, mwenye umri wa miaka 28  baada ya kujifungua mtoto huyo, huku akikata roho. Aidha habari zinasema kuwa, hadi mwanamke huyo anatiwa kitanzi, hakuna aliyekuwa anajua kwamba alikuwa na ujauzito wa miezi saba, kutokana na unene wa mwili wake, suala ambalo limezidi kuwashangaza watu. Sabah alihukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa sumu mumewe na watoto wake wawili na alisalia gerezani kwa muda wa miezi mitatu akisubiri hukumu dhidi yake. Duru za habari zinasema kuwa, watu walishangaa baada ya kuwekwa kamba ya kitanzi shingoni mwake na kufyatuliwa kitanzi, kama ishara ya kumalizika adhabu hiyo, lakini Mosilibasa aliendelea kutikisika miguu licha ya kwamba adhabu hiyo ilikuwa imemashatekelezwa dhidi yake. Muda mchache baadaye alizaa mtoto wa kiume ambaye awali alidhaniwa kuwa naye ameshakufa, lakini baada ya kumsaidia pumzi mtoto huyo aliweza kupumua na kisha kupiga ukelele

Advertisements

ZANZIBAR YAKIRIMIWA WATAALAMU WA KILIMO NA UVUVI KUTOKA VIETNUM

Balozi wa Vietnam Nchini Tanzania Bwana Nguyen Thanh Nam akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na kumpa Taarifa ya ujio wa wataalamu wa Kilimo na Uvuvi wa Vietnam Zanzibar Mwezi Januri mwaka 2014.

Balozi wa Vietnam Nchini Tanzania Bwana Nguyen Thanh Nam akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na kumpa Taarifa ya ujio wa wataalamu wa Kilimo na Uvuvi wa Vietnam Zanzibar Mwezi Januri mwaka 2014.

Timu ya Wataalamu mabingwa katika Sekta ya Kilimo na Uvuvi kutoka Nchini Vietnam inatarajiwa kutembelea Visiwa vya Zanzibar kuanzia Tarehe 4 Mwezi Januari mwaka 2013 kuangalia maeneo ambayo Nchi hiyo inaweza kusaidia Taaluma ili kunyanyua uchumi wa Zanzibar.

Ujio wa Timu hiyo ya wataalamu wa Vietnam unafuatia ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Sheni aliyoifanya Nchini humo miezi michache iliyopita.

Balozi wa Vietnam Nchini Tanzania Bwana Nguyen Thanh Nam Alitoa taarifa hiyo wakati alipofika nyumbani kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Mtaa wa Haile Selassie Jijini Dar es salaam.

Balozi Nguyen alisema ziara ya Rais wa Zanzibar imefungua ukurasa mpya wa uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu ulipo kati ya Vietnam na Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.

Alisema Zanzibar na Vietnam zina wajibu wa kuendelea kushirikiana kwa vile zinafanana katika harakati zao za maendeleo hasa kwenye sekta ya Kilimo na akatolea mfano kile kilimo cha mpunga.

Naye makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameipongeza Nchi hiyo kwa uwamuzi wake wa kukubali kuisaidia Zanzibar kitaaluma katika sekta muhimu za Kilimo na Uvuvi ambazo ndio zenye kubeba idadi kubwa ya wananchi katika kujiendeleza kimaisha.

Balozi Seif alisema Vietnam imekuwa Nchi maarufu Duniani katika uzalishaji wa zao la mpunga ambalo pia wataalamu wake wanaweza kusaidia wakulima wa Zanzibar kuendeleza zao hilo kwa vile ndio chakula kikuu cha wakaazi wa Visiwa vya Zanzibar.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikutana kwa mazungumzo na Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo Nchini Tanzania Bw. Lu Youqing nyumbani kwake Mtaa wa Haile Selassie Jijini Dar es salaam.

Katika mazungumzo yao Viongozi hao wawili wamekubaliana kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya pande hizo mbili rafiki mara tu baada ya  Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisisitiza kuwa uhusiano huo umezidi kupanuka kufuatia pande hizo mbili kusaini mkataba wa ushirikiano katika masuala ya Utamaduni na Michezo.

Balozi Seif alisema mkataba huo hivi sasa umetoa fursa kwa vijana wa pande hizo mbili kuendelea kujifunza tamaduni za kila upande ambazo zimeshaonyesha mafanikio makubwa ya uhusiano huo wa kidugu.

“ Wapo vijana wetu waliopata fursa ya kujifunza tamaduni za ndugu zetu wa China hasa katika mambo ya sarakasi. Lakini kwa upande wao wamepata kujifunza ngoma zetu za utamaduni “. Alisisitiza Balozi Seif.

Naye Balozi wa Jamuhuri ya Watu wa China Nchini Tanzania Bwana Lu Youqing alifahamisha kwamba katika kudumisha uhusiano wa pande hizo mbili Serikali ya Nchi hiyo inakusudia kutuma ujumbe mzito wa Kiserikali kushiriki katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 50 sawa na Nusu Karne ya Mapinduzi ya Zanzibar mwezi Januri mwaka ujao.

Bwana Lu alisema Wananchi wa Zanzibar wana haki ya kujivunia  Mapinduzi hayo matukufu yaliyoondoa madhila na uonevu na yamekuwa kigezo kizuri kilichopatikana  katika kudumisha maendeleo miongoni mwa Wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba.

Aidha Balozi Lu Youqing alieleza kwamba ujumbe wa Viongozi 80 wa Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China ujatarajiwa kuja Nchini Tanzania hivi karibuni kushiriki kongamano la Kimataifa litakalojumuisha Wakuu wa Mikoa wa Tanzania.

Kongamano hilo kubwa limelenga kuwajengea uwezo wa kiutendaji Wakuu hao wa Mikoa ya Tanzania katika masuala mbali mbali ya utawala, Utumishi pamoja na uwajibikaji kwa wananchi.

 

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

DR. MALIK KUPELEKWA INDIA KWA MATIBABU ZAIDI

Mkurugenzi wa hospitali ya Mnazi Moja Dr. Malik akiwa mejeruhiwa na majambazi na kulazwa hospitali ya Jomo Kanyatta nchini Kenya

Mkurugenzi wa hospitali ya Mnazi Moja Dr. Malik akiwa mejeruhiwa na majambazi na kulazwa hospitali ya Jomo Kanyatta nchini Kenya

Mkurugenzi wa hospitali ya Mnazi Mmoja Dr. Malik Abdala Juma aliejeruhiwa vibaya na majambazi mjini Nairobi Kenya anaweza kusafirishwa nje ya nchi hiyo kwa matibabu zaidi.

Akizungumza na Zenji Fm radio naibu waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Abdala Juma Sadala amesema atazungumza na serikali kuangalia uwezekano wa kupelekwa India kwa kupatiwa matibabu zaidi.

Amesema Dr. Malik ameumia sehemu ya kichwa na kuathirika jicho na ubongo na anazungumza kwa taabu.

Hata hivyo amesema amefanyiwa operesheni kubwa na vipimo vimeonesha yuko hali nzuri

Dr. Malik alipoteza mawasiliano na wenzake waliokuwa wakishiriki mkutano wa afya uliowahusisha wakuu wa hospitali na wataalamu tokea siku ya Ijumaa.

DR. MALIK AJERUHIWA NA MAJAMBAZI MJINI NAIROBI

Mkurugenzi wa hospitali ya Mnazi Moja Dr. Malik akiwa mejeruhiwa na majambazi na kulazwa hospitali ya Jomo Kanyatta nchini Kenya

Mkurugenzi wa hospitali ya Mnazi Moja Dr. Malik akiwa mejeruhiwa na majambazi na kulazwa hospitali ya Jomo Kanyatta nchini Kenya

Mkurugenzi Mkuu wa wizara ya afya Zanzibar na  Daktari Bingwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Dr. Malik Abdalla Juma amelazwa katika hospitali ya Kenyatta jijini Nairobi baada ya kujeruhiwa vibaya na majambazi.

Dkt. Malik alikuwa Nairobi kikazi na alipotea tangu Ijumaa iliyopita na hakukuwa na mawasiliano nae, wahusika wa hoteli aliyofikia pia hawakuwa wakifahamu alipo mgeni wao.

USHINDI WA CUF 2015-MAALIM SEIF

DDDChama cha wananchi CUF kimewataka wafuasi wake kujiandaa na ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa kile ilichodai mabadiliko ya uongozi katika nchi za Afrika.

Akihutubia mkutano wa hadhara wa CUF jimbo la Dimani katibu mkuu Malim Seif Sharif Hamad amesema serikali ya umoja wa kitaifa itaendelea kuwepo, lakini kigezo cha chama ni kupata urais.

Aidha amesema chama hicho kitaendeleza ushinfi wa majimbo 18 ya Pemba na mengine manne ya Unguja na ushindi huo utaifanya CUF kuwa na viti 34 vya ujumbe wa baraza sawa na asilimia 70 ya mawaziri.

Malim Seif amedai hata kama baadhi ya vyama vitafanya hilba katika upigaji wa kura, lakini katika uchaguzi ujao  wapiga kura wao watakipigia kura chama cha CUF

Malim Seif amedai hatua ya ushindi wa chama hicho itatokana na mabadiliko ya uongozi katika nchi za Afrika yalioanzia Kaskazini mwa bara hilo.

Katika mkutano huo chama hicho kimepata wanachama wapya 144 walikabidhiwa kadi za CUF na kadi saba za chama cha mapinduzi CCM zilirejeshwa

CCM HAITOUNGANA NA CUF-DR. SHEIN

CCMMAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Mh: dk Ali Mohamed Shein amesema CCM, haijaungana na wala haina nia ya kuunga na chama cha wananchi CUF kisiasa kama baadhi ya watu wanavyodhani.

 

Alisema kilichofanyika ni kuwepo kwa Serikali ya umoja wa kitaifa ‘SUK’ katika utendaji wa kazi ngazi ya serikalini, na sio kuungana na chama hicho kisiasa.

 

Makamu Mwenyekiti huyo alitoa tamko hilo jana, wakati alipokua akizungumza na wanaccm, wapenda amani na wananchi wa Jimbo la Tumbe wilaya ya Micheweni Pemba, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku sita kisiwani humo.

 

Alisema sio kweli kuwa CCM hivi karibuni, kimeungana na Chama cha wananchi CUF kisiasa, bali kilichojitokeza na kushirikiana katika kuanzisha serikali ya umoja wa kitaifa, ambapo hilo liliendana na marekebisho ya katiba ya Zanzibar.

 

Alieleza kuwa katika uwepo wa Serikali hiyo ya Umoja wa kitaifa bado sera na mipango inayotekelezwa ya chama cha Mapinduzi ambacho ndio chama tawala kwa muda mrefu sasa.

 

Aliongeza kuwa katika hilo, CCM kinawanachama wake, sera zake na mipango yake ya kila siku, kama kilivyo chama hicho cha CUF na kubainisha kuwa hakuna pahala waliposaini kuungana kisiasa.

 

‘’Tanzania vipo vyama vya siasa 19 na vinaweza kuzidi, lakini CCM hakuna hata chama kimoja nchini kilichounga na mwalimu wa demokrasia CCM, bali sisi tupo kimpango wetu’’,alifafanua.

 

Katika hatua nyengine Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar, alisema pia kuanzishwa kwa mfumo huo wa vyama vingi nchini, haukuja kwa ajili ya kufanyiana vitishio, kudharauliana wala kubaguana kama baadhi ya wengine wanavyofanya.

 

Alieleza kuwa katika siku za hivi karibuni, kumeibuka viongozi wengine kutoka serikalini, wamekuwa wakiwafanyia vitisho masheha, kwa kuwalazimisha kimaneneo kutoa barua za kupata kitambulisho vya uzanzibari ukaazi.

 

Alifafanua kua wanachokifanya masheha ni kufuata sheria, baada ya kuelekezwa na taaisis husika, hivyo sio busara kwa viongozi hao kuwaona masheha kama wanakiuka sheria.

 

‘’Suala hili la vitambulisho vya uzanzibari ukaazi, tafadhalini msilihusishe na na vyama vya siasa, hili ni la serikali na linatambulika kikatiba na sio la upande mmoja’’,alisema.

 

Aidha Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar ambae pia ni rais wa Zanzibar dk Ali Mohamed Shein, amewataka wananchi kuendelea kuyathamini na kuyaenzi mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

 

Alisema mapinduzi hyo, ndio yaliomkumboa mwanachi wa taifa hili na leo hii, kua ameweza kujitea maendeleo yake mwenyewe na kupata furasa kadhaa zikiwemo za kiuchumi.

 

Alitolea mfano kwa serikali hii ya awamu ya saba inayoongozwa na yeye, kuwa imeamua kulipandisha hadhi zao la karafuu ambalo kwa muda mrefu wakulima walikuwa wamelisahau na kutoona faida yeyote.

 

Hata hivyo amewataka wanaccm hao na wananchi wa Jimbo la Tumbe, wilaya ya Micheweni  kuendelea kuwapuuza wale wanaobeza na kudharau Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

 

Alifafanua zipo fursa kadhaa zilizopatika kwa Zanzibar kupitia Muungano huo, ikiwa ni pamoja na kujenga umoja na udugu kwa muda mrefu.

 

Mapema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa kaskazini Pemba Mberwa Hamad Mberwa, amempongeza makamu mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar, kutokana na kuendelea na utekelezaji wa ahadi zake.

 

Alisema katika Jimbo hilo la Tumbe wananchi kadhaa wamekuwa wakifikiwa na huduma muhimu za kijamii ikiwa ni pamoja na huduma ya maji safi na salama, umeme, elimu ingawa baadhi ya huduma hizo zinahitilafu ndogo ndogo.

DR. SHEIN AWAONYA MASHEHA WANAOWANYIMA WANANCHI VITAMBULISHO VYA UKAAZI

SHEINRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza kuwa suala la Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi ni suala la kisheria hivyo wananchi wenye malalamiko ya kunyimwa vitambulisho hivyo hawana budi kufuata utaratibu wa kisheria wa kukata rufaa ili kudai haki yao hiyo.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa Kaskazini Pemba jana Dk. Shein alieleza kuwa kitambulisho cha Mazanzibari Mkaazi ni suala la mtu binafsi hivyo kila mwenye malalamiko anapaswa yeye binafsi kufuata utaratibu huo.
“Ni suala la kisheria na ni la mtu binafsi hivyo kila anayeamini kuwa amenyimwa kitambulisho hicho kinyume na utaratibu anapaswa kufuata utaratibu wa kisheria wa kukata rufaa si vinginevyo” aliwaeleza mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Alieleza kuwa hakuna mwenye mamlaka ya kumnyima mwananchi kitambulisho hicho si sheha wala mamlaka ya vitambulisho hivyo ikitokea hivyo utaratibu uko wazi kwa mwananchi kukata rufaa kwa waziri husika na kama hakuridhika na uamuzi wa waziri anayo haki ya kukata rufaa kwa Mahkama ya rufaa.
“Suala hili si la Rais ni la kisheria endapo mwananchi haridhika na uamuzi wa kumyima kitambulisho akate rufaa kwa Waziri na asiporidhika aende mahkama ya rufaa”alieza.
Katika mkutano huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alieleza kushangazwa na baadhi ya viongozi kulichukua suala la baadhi ya watu kukosa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi kama njama za kulinyima kundi fulani la watu katika jamii na kutaka malalamiko yao yapatiwe ufumbuzi kinyume na utaratibu wa kisheria uliopo.
“Badala ya viongozi kuwasaidia kwa kuwaelimisha wananchi juu ya utaratibu wa kupata haki yao hiyo baadhi yao kwa bahati mbaya wanawapotosha” Dk. Shein alieleza na kusisitiza kuwa suala hilo “Ni la mtu binafsi lisifanywe kuwa la kundi fulani ili lipatiwe ufumbuzi tofauti na ule wa kisheria”
Akifafanua kuhusu utaratibu wa kupata vitambulisho hivyo Dk. Shein alieleza kuwa pamoja na masharti mengine ni kwa mwananchi kukaa katika eneo husika kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu (miezi 36) na kama ni mtu wa kwenda na kurudi ni jukumu la mkaazi kumthibitishia hilo Sheha wa eneo lake