Rais wa Jamhuri ya muungano Tanzania Jakaya Kikwete

Rais wa Jamhuri ya muungano Tanzania Jakaya Kikwete

Rais wa Jamhuri ya muungano Tanzania Jakaya Kikwete amesema serikali haijafurahia kitendo cha baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuitenga Tanzania katika masuala ya kiuchumi.

 Akiwahutubia wananchi kupitia bunge mjini Dodoma amesema ameshangazwa na hatua ya nchi tatu za Kenya, Uganda na Rwanda kusaini mikataba ya ushirikiano ya miradi iliyomo kwenye mipango jumla, lakini haifikirii kujiengua.

 Amesema kumekuwepo na baadhi ya mambo yaliotajwa kikwazo cha kuendeleza jumuiya hiyo likiwemo suala la kukataa kuharakisha shirikisho, masuala ya ardhi, ajira na uhamiaji

 Aidha amesema hatua kama hiyo itadhoofisha jumuiya na huenda hata ikatishia mustakabali mzuri na wenye matumaini wa watu wa Afrika Mashariki.

Amesema jumuiya hiyo haiwezi kutengamaa bila ya kuwepo misingi ya kiuchumi ikiwemo soko la pamoja, ushuru wa forodha na sarafu ya pamoja sekta ambazo hazijaimarika.

Rais Kikwete ametoa kauli hiyo kuhusu msimamo wa Tanzania juu ya kutengwa na nchi wanachama za Rwanda, Uganda na Kenya.

 Amesema iwapo Jumuiya ya Afrika mashariki itadhofika au kufa Tanzania haitaonyoshewa kidole kama chanzo, lakini itaendelea kumbusha umuhimu wa kuimarishwa kwake.  

Advertisements