Mkurugenzi wa Kituo cha Inter Connection cha clabu ya Rotary Mjini Seattle Bwana Charles Brennick akitoa ahadi Mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na ujumbe wake walipotembelea kituo hicho ya kusaidia kompyuta kwa ajili ya Skuli za Zanzibar. Kushoto ya Bwana Charles ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui.

Mkurugenzi wa Kituo cha Inter Connection cha clabu ya Rotary Mjini Seattle Bwana Charles Brennick akitoa ahadi Mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na ujumbe wake walipotembelea kituo hicho ya kusaidia kompyuta kwa ajili ya Skuli za Zanzibar.
Kushoto ya Bwana Charles ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazrui.

Klabu ya Rotary inayojishughulisha na kituo cha Uungaji na Matengenezo ya Kompyuta katika Mji wa Seattle Nchini Marekani imemua kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Kompyuta 2,500 kwa ajili ya matumizi ya Skuli mbali mbali Visiwani Zanzibar.

Mkurugenzi wa Kituo cha Inter Connection cha clabu hiyo Bwana Charles Brennick alitoa tamko hilo wakati wa Ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea karakana ya Kituo hicho iliyopo kati kati ya Mji wa Settle.
Bwana Carles alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Ujumbe aliofuatana nao wakiwemo Mawaziri na  wafanyabiashara tofauti  kwamba msaada huo utatolewa kwa awamu ambapo ile ya kwanza inatarajiwa kuingia Zanzibar hivi karibuni
Alifahamisha kwamba Taasisi yao imejipangia kutoa misaada kama hiyo kwa Mataifa mbali mbali yanayoendelea Duniani hasa Barani Afrika ambapo  karibu vituo 20 Nchini Tanzania vinaendelea kufaidika na mpango huo.
Mkurugenzi huyo wa Inter Connection alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais kwamba licha ya kwamba Zanzi bar iko mbali Kijiografia kutoka eneo hilo lakini Uongozi wa Taasisi hiyo umejikita katika kuona msaada huo wa Kompyuta unafika Zanzibar  kwa wakati walioupangia.
Naye kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliushukuru Uongozi wa Taasisi hiyo kwa uamuzi wake wa busara wa kuona umuhimu wa kuisaidia Zanzibar nyenzo hiyo.
Balozi Seif alieleza kwamba matumizi ya kompyuta sambamba na  mitandao ya mawasiliano ya internet yaliyosambaa hivi sasa ulimwenguni ndio yanayowapa fursa nzuri wanafunzi kuweza kumudu vyema na kisasa masomo yao.
Alifahamisha kwamba msaada huo wa kompyuta umekuja wakati muwafaka kwa wanafunzi wa Zanzibar kuelekea katika mazingira ya kimafunzo yanayokwenda na wakati kufutia mabadiliko ya sasa ya dunia ya sayansi na Teknolojia.
“ Furaha iliyoje kwetu sisi hasa wanafunzi wetu wanaposikia tunaungwa mkono tena katika masuala yanayowahusu wao watoto wetu. Tunaamini kwamba msaada huu utasaidia Vijana wa Zanzibar kwenda na wakati kutokana na mabadiliko ya Dunia “. Alisisitiza Balozi Seif Ali Iddi.
Baadaye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikutana na ujumbe aliofuatana nao katika Ukumbi wa Hoteli ya Kimataifa ya Marriot kupanga mikakati ya muelekeo wa itakavyokuwa ziara yao ya wiki moja Mjini Settle Nchini Marekani.
Balozi Seif aliwasili kwenye uwanja wa wa ndege wa Kimataifa ya Seattle mapema mchana akitokea Dubai akitarajiwa kuhudhuria mkutano wa 15 wa Chama cha Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika katika Jimbo la Seattle.
Mkutano huo unatarajiwa pia kuhudhuriwa na baadhi ya waalikwa kutoka Taasisi tofauti za Kimataifa za Kibiashara katika mataifa mbali mbali Duniani wakiwemo pia baadhi ya Viongozi wa Jumuiya za wafanyabiashara kutoka Barani Afrika.
Ziara hiyo itatoa fursa maalum kwa wafanyabiashara wa Zanzibar kukutana na wenzao wa Mji huo katika kujenga mazingira ya ushirikiano na urafiki wa kibiashara kati ya pande hizo mbili
Advertisements