DDDChama cha wananchi CUF kimewataka wafuasi wake kujiandaa na ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa kile ilichodai mabadiliko ya uongozi katika nchi za Afrika.

Akihutubia mkutano wa hadhara wa CUF jimbo la Dimani katibu mkuu Malim Seif Sharif Hamad amesema serikali ya umoja wa kitaifa itaendelea kuwepo, lakini kigezo cha chama ni kupata urais.

Aidha amesema chama hicho kitaendeleza ushinfi wa majimbo 18 ya Pemba na mengine manne ya Unguja na ushindi huo utaifanya CUF kuwa na viti 34 vya ujumbe wa baraza sawa na asilimia 70 ya mawaziri.

Malim Seif amedai hata kama baadhi ya vyama vitafanya hilba katika upigaji wa kura, lakini katika uchaguzi ujao  wapiga kura wao watakipigia kura chama cha CUF

Malim Seif amedai hatua ya ushindi wa chama hicho itatokana na mabadiliko ya uongozi katika nchi za Afrika yalioanzia Kaskazini mwa bara hilo.

Katika mkutano huo chama hicho kimepata wanachama wapya 144 walikabidhiwa kadi za CUF na kadi saba za chama cha mapinduzi CCM zilirejeshwa

Advertisements