NUSU UCHIWizara ya habari, utamaduni, utalii na michezo imewataka wanachi kuwafikisha katika vituo vya polisi watu wanaovaa mavazi ya nguo za nusu uchi na zinazobana.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi waziri Said Ali Mbarouk amesema sheria namba moja ya mwaka 1973 inatoa fursa kwa wananchi kusimamia utekelezaji wake kwa kuwafikisha vituo vya polisi watu wanavaa nguo zinazokwenda na sheria hiyo… 

Aidha Mbarouk amesema sheria hiyo pia inatoa fursa kwa wananchi kuwakamata wanaume wanaovaa mapambo ya kike ikiwemo herini, kidani na kusuka nywele kuwafikisha vituo vya polisi.

Advertisements