Khamis Kagasheki

Khamis Kagasheki

Waziri wanne wa serikali ya Jamhuri ya muungano Tanzania wamejiuzulu wadhifa wao baada ya kutokea mjadala mkali ndani ya bungeni mjini Dodoma.

Mawaziri waliojiuzuu ni waziri wa maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki, waziri wa mambo ya ndani Dr. Emanuel Nchimbi, waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Shamsi Vuai Nahodha na waziri wa mifugo na uvuvi Dr. Matayo David Matayo.

Kwa muibu wa taarifa ya waziri mkuu Mizengo Pinda mawaziri hao wametoa taarifa ya kujiuzulu nyadhifa zao baada ya kuwasilisha barua zao za kujiuzulu.

Akizungumza bungeni juu ya hatua yake hiyo Kagasheki amesema licha ya kutangaza kujiuzulu, lakini bado ataendelea kulitumikia taifa

Nae mbunge wa chama cha TLP Augostino Mreme akitoa maoni yake juu ya kujiuzulu kwa mawaziri hao amewapongeza mawaziri hao kwa kile alichokieleza kuwajibi kwa vitendo.

Aidha Mrema amewata mawaziri wengine wanaotajwa kutotimiza majukumu yao vizuri wajitokeze na kutangaza kujiuzuu badala ya kuendelea kungania madaraka

Hatua hiyo ya kujiuzulu imekuja baada ya chama tawala CCM kuwasilisha mapendekezo kwa rais Kikwete kuhusu mawaziri saba waliotajwa kutofikia malengo ya ilani ya chama hicho.

Hata hivyo habari zaidi zinasema rais wa jamhuri ya muungano Tanzania Jakaya Kikwete amebariki hatua ya kujiuzulu kwa mawaziri hao

Advertisements