Mwakilishi wa jimbo la Wete CUF Asaa Othman

Mwakilishi wa jimbo la Wete CUF Asaa Othman

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshauriwa kutunga sheria itakayotoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa mtu atakaepatikana na hatia ya kumbaka au kumlawiti mtoto mdogo.

Mwakilishi wa jimbo la Wete Asaa Othman  amesema ingawa mataifa ya nje yataingilia kati sheria hiyo kwa madai ya haki za binadamu, lakini watu wanaofanya vitendo hivyo ndio  wanavunja haki hizo.

Akichangia hoja bainafsi  ya azimio la vitendo vya udhalishaji wa watoto amesema adhabu hiyo ikiambatana na viboko 50 ndio itakayomaliza tatizo la vitendo vya udhalilishaji dhidi ya watoto Zanzibar.

        Aidha Hamad amesema wazazi watakaoficha vitendo vya udhalilishaji kwa kuhofia jamaa zao kupelekwa  vyombo vya sheria amependekeza wapewe adhabu ya kifungo cha miaka 10 jela 

Hoja hiyo binafsi iliyowasilishwa jana na mwakilishi wa viti Maalum Mgeni Hassan Juma ina lengo la kuanzisha sheria na mikkati itayosaidia kukomesha vitendo vya udhalishaji dhidi ya watoto vinavyongezeka

Advertisements