Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Zanzibari 2013

Jaji Joseph Warioba Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Tanzania 2013

Tume ya mabadiliko ya katiba Tanzania imependekeza kuwepo kwa muundo wa  Serikali tatu ili pande zote mbili za jamuhuri ya mungano ziwe na hadhi sawa .

Katika Mapendekezo hayo  kila upande utashughulikia mambo yasiyo ya muungano na serikali ya muungano itabaki na mambo machache ya msingi ambayo yanaunganisha taifa.

Akiwasilisha ripoti ya Rasimu ya pili ya katiba kwa rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohammed Shein Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba katika viwanja vya Ukumbi wa Karimjee jijini Dare s salaam.

Katika taarifa hiyo imesema Ili kujikinga na changamoto katika muundo huo tume imependekeza uraia uwe mmoja na raia wote wa jamuhuri wawe na uhuru na wawe na haki zote za siasa ,kiuchumi,  kijamii katika nchi nzima isipokuwa katika mazingira maalum.

Ripoti hiyo imesema kuwa iwapo haki zao zikiingiliwa na upande wowote bila ya sababu maalum kutapelekea kuibuka kwa utaifa na uzalendo utajumba.

Kwa upande wake Rais Jakaya Kikwete amesema umuhimu wa kuichapisha rasimu hiyo katika gazeti la serikali zaidi upo kwa walengwa ambao ni wajumbe wa bunge la Katiba ambao ndio wenye dhamana kubwa ya kuijadili rasimu hii na kuiimarisha kwa kuifanya marekebisho pale panapostahiki.

Nae Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein amesema tokea kuanza kwa hatua za mabadiliko  ya katiba Serikali zote mbili zimejifunza zaidi kero na changamoto za mambo ya muungano na yasiyokuwa na muungano ambayo yanagusa maisha ya wananchi wote

Advertisements