Archive for January, 2014

WABUNGE KUJIONGEZEA MAMILIONI

BUNGE LA TANZANIAWachambuzi wa masuala ya kiuchumi Tanzania wameishutumu hatua ya wabunge ya kujiongezea malipo ya kumaliza kipindi chao cha ubunge mwaka 2015.

Wizara ya fedha Tanzania na ofisi ya waziri mkuu zimeidhinisha malipo ya shilingi milioni 160 kwa kila mbunge ikiwa ni ongezeko la malipo ya mara tatu zaidi yaliokuwa yakitolewa ya shilingi milioni 43.

Mbunge wa kuteuliwa na mwenyekiti wa taifa wa chama cha NCCR-MAGEUZI, James Mbatia amesema nyongeza hiyo inazidi kuongeza umasikini kwa watanzani

Advertisements

VIONGOZI WA UAMSHO WAMEPEWA DHAMANA KWA MASHARTI

Na Mauwa Mohammed Zanzibar
uamshoMahkama kuu Vua Mjini Zanzibar imetoa dhamana ya masharti magumu kwa viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na mihadhara ya Kislamu
Akitoa mamuzi hayo Jaji wa mahkama hiyo Fatma Hamid  Mahmoud amewataka kuwasilisha fedha shilingi milioni 25 taslim ,wadhamini watatu wakiwa ni wafanyikazi wa Serikali ya (SMZ) kati yao moja awasilishe mali isiyohamishika yenye thamani ya fedha kama hizo.
Mashti mengine ni pamoja na Kuwasilisha vitambulisho na Pasi za kusafiia mahkamani hapo,kutotoka nje ya Zanzibar,kutofana mihadhaa ndani na nje ya misikiti,kutofanya vitendo vyovyote venye kuashiria fujo kinyume na hilo watarudi rumande hadi kesi itakapokwisha.
Mapema mwendesha mashitaka wa serikali aliwasilisha pingamizi  mbele jaji huyo za kuzuwia amri ya kuwataka kuwasilisha sababu za kuzuwia dhamana za watuhumiwa hao.
Watuhumiwa hao ni  Farid Hadi Ahmed (41) mkaazi wa Mbuyuni,Mselem Ali Mselem (52) mkaazi wa Kwamtipura, Mussa Juma Mussa (47) mkaazi wa Makadara na Azan Khalid (48) mkaazi wa Mfenesini.
Wengine ni Suleiman Juma Suleiman (66), mkaazi wa Makadara, Khamis Ali Suleiman (59) mkaazi wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakar Suleiman (39) mkaazi wa Tomondo, Ghalib Ahmada Juma (39) mkaazi wa Mwanakwerekwe , Abdallah Said (48) mkaazi wa Misufini na Majaliwa Fikirini Majaliwa
.Mashtaka waliosomewa washitakiwa hao ni kuharibu mali,  Uchochezi,Ushawishi na kuhamasisha fujo na kosa la tatu ni kula njama ya kufanya kosa
Kosa la nne likimkabili mshitakiwa namba nne Azan Khalid
ambae anadaiwa kutoa maneno ya matusi kwa kamishna wa polisi vitendo vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Vitendo hivyo vinadaiwa   kufanyika kati ya Oktoba 17,18 na 19 katika maeneo tofauti katika manispaa a mji wa Zanziba ambapo washitakiwa hao wote walikana makosa yote hayo .
Kesi hiyo iliakhirishwa  hadi februai 27 mwaka huu na watuhumiwa walirudi rumande hadi watakapokamilisha masharti ya dhamana zao

PROFISA LIPUMBA AMESEMA WAZIRI WA FEDHA SAADA MKUYA ELIMU YAKE INATIA MASHAKA

Waziri wa fedha Tanzania Saada Mkuya

Waziri wa fedha Tanzania Saada Mkuya

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amelishushia tuhuma nzito Baraza la Mawaziri, baada ya kudai baadhi ya mawaziri walioteuliwa hawana elimu ya kutosha
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mmoja wa mawaziri hao ni Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.

Alisema chama chake, kina wasiwasi na elimu ya Waziri Mkuya, kutokana na wasifu wake kutoonyesha vyuo alivyosoma wakati wa kupata shahada ya kwanza na ya pili katika masuala ya biashara.


Alisema katika tovuti ya Bunge, wasifu wa waziri huyo umeonyesha sehemu aliyosoma elimu ya sekondari na kuhitimu kidato cha sita.


Alisema katika tovuti hiyo, haionyeshi chuo alichosoma shahada ya kwanza ya biashara, ingawa inaonyesha masomo aliyochukua jambo ambalo linatia mashaka uhalali wake kuongoza wizara hiyo nyeti.


“Ukiingia kwenye tovuti ya Bunge, utaona wasifu wake kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha sita na shule alizosoma, lakini kuanzia elimu ya shahada imeonyesha masomo aliyochukua na kupata shahada ya kwanza ya biashara, haionyeshi vyuo, jambo ambalo linatia mashaka,” alisema Lipumba.

Alisema nafasi aliyopewa inahitaji kiongozi mwenye upeo wa hali ya juu, kuweza kupambanua mambo yanayohusu uchumi wa nchi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha za ndani na nje ya nchi.

“Napata wasiwasi kama Rais Jakaya Kikwete, aliangalia wasifu wa waziri wake kwa sababu asingeweza kumchagua kushika nafasi kubwa kama hii, wakati vyeti vyake vina mashaka,” aliongeza.


Alisema kitendo cha kumuweka mtu mwenye vyeti vya mashaka, kunaweza kusababisha nchi kuyumba kiuchumi, kuongezeka kwa deni la taifa, kwa sababu uamuzi wake unatokana na ufahamu wake.

WAZIRI AJIBU

Akizungumza na MTANZANIA Jumatatu kuhusu madai hayo, Waziri Mkuya alisema elimu yake wala haina mashaka, kwani alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Lumumba mjini Zanzibar.


Baada ya hapo, alijiunga na masomo ya diploma ya Biashara katika Chuo cha Stamford cha Malaysia, ambapo pia alichukua diploma nyingine ya biashara nchini Uingereza.


Alisema mbali na masomo hayo, pia amesoma shahada ya pili ya biashara katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na kuhitimu mwaka 2009.

“Nimehitimu Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara (MBA) ya Chuo Kikuu cha WATT kilichopo Edinburgh, Scotland.

“Kwa sasa nachukua Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Utawala wa Biashara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, tawi la Dar es Salaam,” alisema Mkuya

MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATU CHA PILI 2013 ZANZIBAR HAYA HAPA BONYENZA HAPA

http://www.moez.go.tz/docs/qhjgN539Hy_WANAFUNZI__WALIOFAULU_KIDATU_CHA_PILI_MWAKA_2013.pdf

RAIS KIKWETE ALIFANYIA MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UHAMISHO NA UTEUZI WA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI
______________________________________________
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:-
1.0 OFISI YA RAIS
Hakuna mabadiliko.
2.0 OFISI YA MAKAMU WA RAIS
2.1 Waziri wa Nchi (Muungano) – Hakuna mabadiliko
2.2 Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb)
Waziri wa Nchi (Mazingira).
2.3 Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb)
Naibu Waziri
3.0 OFISI YA WAZIRI MKUU
Hakuna mabadiliko
4.0 WIZARA
4.1 WIZARA YA FEDHA
4.1.1 Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb)
Waziri wa Fedha
Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)
Naibu Waziri wa Fedha
4.1.2 Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)
Naibu Waziri wa Fedha
4.2 WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Hakuna mabadiliko
4.3 WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
4.3.1 Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)
Waziri wa Katiba na Sheria
4.3.2 Naibu Waziri – Hakuna mabadiliko
4.4 WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Hakuna mabadiliko
4.5 WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
4.5.1 Waziri – Hakuna mabadiliko
4.5.2 Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb)
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
4.6 WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA
Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
4.7 WIZARA YA UJENZI
Hakuna mabadiliko
4.8 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
4.8.1 Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)
Waziri wa Mambo ya Ndani
4.8.2 Naibu Waziri – Hakuna Mabadiliko
2
4.9 WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
4.9.1 Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
4.9.2 Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
4.10 WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
4.10.1 Waziri: Hakuna mabadiliko
4.10.2 Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb)
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
14.11 WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
14.11.1 Waziri: Hakuna mabadiliko
14. 11.2 Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
14.12 WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
14.12.1 Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb)
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
14.12.2 Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
14.13 WIZARA YA KAZI NA AJIRA
Hakuna mabadiliko
14.14 WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Hakuna mabadiliko
14.15 WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
14.15.1 Waziri – Hakuna mabadiliko
14.15.2 Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
14.16 WIZARA YA MAJI
14.16.1 Waziri – Hakuna mabadiliko
3
14.16.2 Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)
Naibu Waziri wa Maji
14.17 WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA
14.17.1 Waziri – Hakuna mabadiliko
14.17.2 Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb)
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
4.18 WIZARA YA UCHUKUZI
Hakuna mabadiliko
4.19 WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
4.19.1 Waziri – Hakuna mabadiliko
4.19.2 Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb)
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
4.20 WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
4.20.1 Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)
Waziri wa Maliasili na Utalii
4.20.2 Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
4.21 WIZARA YA NISHATI NA MADINI
4.21.1 Waziri – Hakuna mabadiliko
4.21.2 Naibu Waziri (Madini) – Hakuna mabadiliko
4.21.3 Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)
Naibu Waziri (Nishati)
Balozi Ombeni Y. Sefue
KATIBU MKUU KIONGOZI
Ikulu
4
DAR ES SALAAM
19 Januari, 2014
5

FUNGAMANENI NA MAISHA MAISHA YA MTUME SAW

900Waumini wa Dini ya Kiislamu popote walipo katika  kipindi hichi cha kusherehekea uzawa wa Kiongozi  wa Dini hiyo Ulimwenguni Mtume Muhammad { SAW } wana wajibu wa kupitisha maazimio ndani ya nafsi zao ya kuachana na maovu na kukumbatia mema yote kama alivyokuwa akiyahubiri Kiongozi huyo wakati wa uhalifa wake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo katika kisomo cha mazazi ya Mtume Muhammad { SAW } kilichofanyika katika ukumbi wa wapenzi wa Mtume Muhammad { SAW } wa Chaurembo waliopo katika Mtaa wa Msimbazi Kariakoo Mjini Dar es salaam.
Balozi Seif alisema mkusanyiko wa waumini wa Kiislamu katika kutukuza uzawa wa Kiongozi wao utakuwa na manufaa makubwa endapo kila muumini atadhamiria kusoma kwa kina maisha ya kiongozi huyo kwa lengo la kufuata mwenendo wake.
Alitoa wito kwa wapenzi wa Mtume  Muhammad { SAW } kufanya utafiti mbali mbali zitakazotoa fursa kwa waumini wa dini ya Kiislamu popote pale kusoma na hatimae kuelewa vyema maisha na mfumo aliokuja nao Kiongozi huyo wa umma wa Kiislamu.
“ Ikiwezekana tafiti hizo ni vyema zikaandikwa kwa lugha ya Kiswahili ili watu wengi zaidi wapate kuzisoma. Kuelewa maisha ya Mtume Muhammad { SAW } ni hatua muhimu kwa muumini wa Kiislamu kuielewa Dini yake “. Alisisitiza Balozi Seif.
“  Akinukuu baadhi ya maandiko yaliyotolewa na  wanafalsafa wa Dini ya Kiislamu Balozi Seif alisema kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad { SAW } ni sawa na kusherehekea kuzaliwa kwa Uislamu “.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwasisitiza waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuwa na utiifu, subra wakati wa matatizo sambamba na kujijengea maisha bora ya milele ambayo kila muumini anayaelewa.
Balozi Seif alielezea faraja yake kutokana na uwepo wa Umoja wa wapenzi wa Mtume Muhammad { SAW } hapa Tanzania ambao unastahiki kupongezwa pamoja na kuungwa mkono .
Alisema jamii katika kipindi kirefu ilikuwa ikishuhudia kuwepo kwa umoja wa wapenzi wa vilabu vya mchezo wa mpira wa miguu au wanamuziki badala ya kuwa na umoja kama huo unaoleta faida pande zote mbili Duniani na Makazi ya milele.
“ Maandalizi ya sherehe hiziyameonyesha wazi kwamba nyinyi kweli ni wapenzi wa Mtume Muihammad { SAW }. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuzidishie mapenzi yetu kwa kiongozi wetu huyo “. Alifafanua Balozi Seif.
Akitoa salamu kwenye hafla hiyo ya kisomo cha mazazi ya Mtume Muhammad       { SAW } Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi alisema waumini wa Dini ya Kiislamu wana wajibu wa Kumshukuru Mola kwa kuupatia umma huu wa mwisho Kiongozi aliyekamilika kwa tabia, nasabu pamoja na Umbo.
Mzee Mwinyi aliwataka waislamu hao kuendelea kuheshimu nema walizopewa na Mwenyezi Mungu za kupatia Kitabu kitukufu na bora chenye mfumo kamili wa kufuatwa na wanaadamu katika maisha yao ya kila siku.
Mapema Mkurugenzi wa Kituo cha Kiislamu kilichopo Tandika Mjini Dar es salaam akiwa miongoni mwa matunda ya chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu cha Al – Akhzal nchini Misri Sheikh Usama Ismail alisema dalili za utukufu wa Mtume Muhammad { SAW } zilianza kujichomoza tokea zama za Mitume waliomtangulia.
Sheikh Usama alifahamisha kwamba Kiongozi huyo wa Umma wa Kiislamu alibashiriwa utukufu wa kuja kwake duniani ambao baadhi ya maulamaa wa enzi zilizopita waliushuhudia ndani ya vitabu vitukufu.
Katika hafla hiyo ya kisomo cha mazazi ya Mtume Muhammad { SAW } Muasisi wa Umoja wa wapenzi wa Mtume Muhammad { SAW } wa Chaurembo waliopo katika Mtaa wa Msimbazi Kariakoo Sheikh Majid aliwapongeza Viongozi hao kwa ukaribu wao na waumini pamoja na wananchi kwenye masuala mbali mbali ya kijamii.
Katika kuunga mkono harakati za kijamii zinazofanywa na viongozi hao Sheikh Majid kwa niaba ya Umoja huo alikabidhi zawadi za Juzuu, Mashafu pamoja na hati maalum kama ukumbusho kwa wageni hao waalikwa akiwemo pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al Hajj Daktari Ali Mohamed Shein.
 
 
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

MAHAMOUD THABIT ACHUKUA FOMU

Mahamoud Thabit KomboMgombea wa CCM katika Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo  leo amechukua  fomu ya kuwa ni uwakilishi na kuwa mgombea watatu huku akisifu  demokrasia ya chama hicho ni adilifu na shirikishi kuliko vyama vingine vya siasa nchini.

Mahmoud ameyaeleza hayo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa fomu  hiyo na Msaimaizi wa Uchaguzi jimbo la Kiembesamaki Suluhu Ali Rashid huko Maisra  akisindikizwa na wanachama wa chama hicho.

Amesema licha ya ukubwa wa  Chama Cha Mapinduzi pia amesema kinajivunia histopria yake hata kabla ya kuungana  kwa vyama vya TANU na ASP mwaka 1977 ambacho kimekuwa mstari wa mbele  kupigania uhuru,usawa  na ukombozi Kusini mwa Afrika.

Aidha ameeleza kuwa uchaguzi  ni shughuili za makundi na ushindani unaofuata miiko,  maadili, nidhamu na katiba ya chama hicho hivyo wanapogombea wanachama wengi mmoja lazima ashinde na kupitishwa.

Mahmoud amesema si kwamba amewashinda wenzake ila kura zake zimetosha huku akiamini atashirikiana na wenzake kuhakikisha CCM inapata ushindi katika uchaguzi huo mdogo

Amesema wako pamoja na kuhakikisha wanakiletea chama hicho  ushindi, na kusema atafanya nitafanya kampeni za kistaarabu,kunadi sera majukwani  na kusimamia misimamo, mipango na miongozo ya CCM

Ameahidi kuendelea kuwa muumini wa mfumo wa  Muungano wa Serikali mbili , mlinzi na  mtetezi wa Mapinduzi ya Zanzibar hadi tone lake la mwisho la damu yake.

Hadi sasa wagombea watatu wamechukua fomu ya kuwania kiti hicho akiwwemo Abdulmalik Haji Jecha wa CUF , Amani Ismail Rashid wa ADC na Mahamoud Thabit Kombo wa CCM