Mahamoud Thabit KomboMgombea wa CCM katika Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo  leo amechukua  fomu ya kuwa ni uwakilishi na kuwa mgombea watatu huku akisifu  demokrasia ya chama hicho ni adilifu na shirikishi kuliko vyama vingine vya siasa nchini.

Mahmoud ameyaeleza hayo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa fomu  hiyo na Msaimaizi wa Uchaguzi jimbo la Kiembesamaki Suluhu Ali Rashid huko Maisra  akisindikizwa na wanachama wa chama hicho.

Amesema licha ya ukubwa wa  Chama Cha Mapinduzi pia amesema kinajivunia histopria yake hata kabla ya kuungana  kwa vyama vya TANU na ASP mwaka 1977 ambacho kimekuwa mstari wa mbele  kupigania uhuru,usawa  na ukombozi Kusini mwa Afrika.

Aidha ameeleza kuwa uchaguzi  ni shughuili za makundi na ushindani unaofuata miiko,  maadili, nidhamu na katiba ya chama hicho hivyo wanapogombea wanachama wengi mmoja lazima ashinde na kupitishwa.

Mahmoud amesema si kwamba amewashinda wenzake ila kura zake zimetosha huku akiamini atashirikiana na wenzake kuhakikisha CCM inapata ushindi katika uchaguzi huo mdogo

Amesema wako pamoja na kuhakikisha wanakiletea chama hicho  ushindi, na kusema atafanya nitafanya kampeni za kistaarabu,kunadi sera majukwani  na kusimamia misimamo, mipango na miongozo ya CCM

Ameahidi kuendelea kuwa muumini wa mfumo wa  Muungano wa Serikali mbili , mlinzi na  mtetezi wa Mapinduzi ya Zanzibar hadi tone lake la mwisho la damu yake.

Hadi sasa wagombea watatu wamechukua fomu ya kuwania kiti hicho akiwwemo Abdulmalik Haji Jecha wa CUF , Amani Ismail Rashid wa ADC na Mahamoud Thabit Kombo wa CCM

 

Advertisements