Waziri Haroun Ali Suleiman

Waziri Haroun Ali Suleiman

                Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema hali ya waziri wake Haroun Ali Suleiman aliepelekwa Afrika ya Kusini kwa matibabu ya maradhi ya moyo inaendelea vizuri na ameanza mazowezi baada ya kufanyiwa upasuwaji.

Taarifa hiyo ya serikali imekuja kufuatia uvumi uliozagaa mitaani kupitia mitandao ya kijamii na ujumbe mfupi wa simu za mkonoi kuwa waziri huyo amefariki dunia jana baada ya hali yake kuwa mbaya.

Akitoa taarifa hiyo katika kikao cha baraza la wawakilishi makamu wa pili wa rais balozi Seif Ali Iddi amesema tarehe Mosi mwezi huu aliwasiliana na balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini  Raziya Msuya na mwanawe Ali Haroun na kusema hali yake inaendelea vizuri.

Amesema waziri Haroun alifanyiwa upasuwaji Januari 21 na hali yake imeimarika baada ya upasuwaji huo na amewataka wanchi kutokuwa na wasiwasi juu ya afya yake.

                Waziri Haroun ambae pia ni mwakilishi wa jimbo Makunduchi alilazwa hospitali ya Mnazimmoja mapema mwezi uliopita kabla ya kupelekwa nchini Afrika ya Kusini kwa matibabu zaidi alihamishiwa hospitali ya Muhimbili.

 

 

                                                                                                12

 

Advertisements