Rashid Yussuf Mchenga akizungumza na wandishi wa habari akiwa katika harakati zake za kisiasa

Rashid Yussuf Mchenga akizungumza na wandishi wa habari akiwa katika harakati zake za kisiasa

Chama cha wakulima AFP kimemfukuza uanachama mkurugenzi wake wa sera na uenezi Rashid Yussuf  Mshenga kwa tuhuma za  kufanya udanganyifu kuingia kwenye bunge la katiba.

Wakizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa AFP taifa na Said Soud na naibu katibu mkuu Shaib Masoud Salum wamesema mwanachama huyo ameghushi saini ya naibu katibu  ili kujiorodhesha kwenye majina waliomba kuwa wajumbe wa bunge hilo kupitia AFP.

Wamesema AFP hakijapitisha jina la Mshenga kuwa miongoni mwa wajumbe wa kuteuliwa na chama kushiriki kwenye bunge la katiba.

Viongozi hao wamesema mwanachama huyo ametumia njia zisizo halali kuwasilisha jina lake katika afisi ya rais Zanzibar.

Aidha chama cha AFP kimepanga kumfungulia mashtaka Mchenga kwa tuhuma za kufanya udanganyifu.

Akizungumza mara baada ya uamuzi huo kutangazwa, Mchenga amesema chimbuko la kuibuliwa mgogoro huo ni Mwenyekiti  wake na mkewe kukosa utezi wa kuwa wabunge la katiba.

Amesma ni choyo cha Mwenyekiti wake pamoja na kuchukizwa kukosa nafasi ya hiyo na sasa ameamua kumchafua katika jamii na kumvunjia heshima yake.

Mchenga media kinachofanyika kati ya Mwenyekiti wake na  Naibu wa chamam hicho Shaibu Masoud Salum ni udugu wao kifamilia.

Mchenga ni miongoni mwa wajumbe wa vyama vya siasa upande wa Zanzibar walioteuliwa na rais Jakaya Kikwete kuingia ndani ya bunge la katiba

Advertisements