DDDMahkama kuu Zanzibar leo imetoa dhamana kwa viongozi 10 wa jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kislamu.

Hatua hiyo ya kupatiwa dhamana imekuja baada ya kupunguza masharti magumu ya kulipa fedha taslimu shailingi milioni 25 na badala yake watalipa kwa maanishi.

Jaji wa Mahkama hiyo Fatma Hamid Mahmoud ametoa uamuzi huo na kusema kwa vile watuhumiwa wameshakaa ndani kwa muda mwingi mahkma imeona wana haki ya kupatiwa dhamna yeney masharti nafuu.

Jaji Fatma alikubali maombi yaliotolewa na mawakili wa watuhumiwa hao wakiongozwa na Salum Toufiq kila mshitakiwa kujidhamini mwenyewe kwa shilingi milioni 25 za mandishi, wadhamini wawili moja akiwa mfanyikazi wa serikali na kuwasilisha nyaraka za mali isyohamishika.

Awali watuhumiwa hao walipewa madharti magumu ya kujidhamini ikiwemo kutoa fedha taslimu shilingi milioni 25, wadhamini watutu watumishi wa serikali moja wao awasilishe mali isiyohamishika masharti ambayo yaliwashinda na kulazimika kurudi tena ndani.

Watuhumiwa hao ni Faraidi Hadi Ahmed, Mselem Ali Mselem, Musa Juma Mussa, Azan Khalid Hamdan, Sleiman Juma Sleiman, Khamis Ali Sleiman, Hasan Bakari Sleiman.

Wengine ni Gharibu Ahmada Juma, Abdalla Saidi na Majaliwa Fikirini Majaliwa wanashtakiwa kw amakosa ya kuharibu mali,  Uchochezi, Ushawishi na kuhamasisha fujo Octoba mwaka 2012.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi  Mach 27 mwaka huu kwa kusikilizwa tena.

Advertisements