Archive for March, 2014

Badozip Zeni

Badozip Zeni

Advertisements

NBA BANK YAKABIDHI MADAWATI 100 SKULI YA DONGE

Meneja wa Tawi la Benki ya NMB Bwana Bakari Khamis Mohd akimkabidhi madeski 50 Mbunge wa Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma Khamis kwa ajili ya Skuli ya Sekondario ya Doonge.

Meneja wa Tawi la Benki ya NMB Bwana Bakari Khamis Mohd akimkabidhi madeski 50 Mbunge wa Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma Khamis kwa ajili ya Skuli ya Sekondario ya Doonge.

Benki ya kuhudumia Wananchi wa Kawaida  Nchini { NMB } imekabidhi mchango wa Vikalio 100 kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu katika Skuli za Sekondari za Donge na Kitope zilizomo ndani ya Wilaya ya Kasakazini “ B “ Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Msaada huo wa Vikalio wenye gharama ya shilingi za Kitanzania Milioni Kumi utasaidia kupunguza uhaba wa madeski kwa Skuli hizo za Donge na Kitope ambapo kila Skuli imefanikiwa kupata madeski 50.

Meneja wa Tawi la NBC Zanzibar Bwana Bakari Khamis Moh’d alikabidhi  msaada huo kwa  Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Donge Mh. Sadifa Juma Khamis hafla iliyofanyika hapo katika skuli ya Sekondari Kitope.

Meneja huyo wa Tawi la Benki ya NMB Bwana Bakari aliiomba Jamii kuendelea kuiunga mkono Benki hiyo ili kusaidia kuipa nguvu za kiutendaji itakaoongeza kasi ya kusaidia harakati za Kijamii Nchini.

Alisema Benki hiyo tokea kuasisiwa kwake mnamo mwaka 1997 imekuwa ikijitahidi kuunga mkono maendeleo ya Wananchi hasa katika miradi iliyomo ndani ya Sekta ya Elimu.

Akitoa shukrani zake mara baada ya kupokea msaada huo wa vikalio Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameziomba Benki nyengine Nchini kuiga mfano wa Benki ya NMB katika kusaidia maendeleo ya Wananchi.

Balozi Seif alisema taasisi za Kifedha ndani na nje ya nchi zimekuwa na mfumo maalum unaosaidia kuunga mkono juhudi za jamii katika maeneo tofauti ya kiuchumi na ustawi wa jamii.

Alisema Wananchi hawanabudi kushirikiana na kuzipa nguvu taasisi hiyo ili ziweze kutekeleza malengo zilizojipangia.

 

“ Ukweli halisi NMB ni Benki ya wanyonge. Ni Benki yetu inayolenga kuhudumia wananachi wa kipato cha chini. Huyu ndie rafiki yetu na tunapaswa kumuunga mkono “. Alisema Balozi Seif.

Naye Mbunge wa Jimbo la Donge  Mh. Sadifa Juma Khamis alisema Benki ya NMB imeonyesha umahiri mkubwa katika kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010  ambayo imejipangia kuimarisha Sekta ya Elimu iliyo  muhimili pekee wa maendeleo ya kiuchumi kwa Taifa lolote Duniani.

Akisoma risala ya Walimu na wazazi wa Skuli za Donge na Kitope Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Kitope Mwalimu Suleiman  Juma Makame ameupongeza Uongozi wa Benki hiyo pamoja na ule wa Jimbo la Kitope kwa juhudi zao zilizojikita zaidi katika kuimarisha Sekta ya Elimu.

Hata Hivyo Mwalimu Suleiman alisema zipo changa moto zinazoendelea kuzikabili skuli hiyo akatolea mfano wa Skuli yake ya Kitope inayokabiliwa na uhaba wa Vifaa vya Maabara pamoja na uwezekwaji wa jengo moja la Skuli hiyo.

Akitoa  salamu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Afisa  Elimu wa Wilaya ya Kaskazini “B “ Mwalimu Ussi Machano alieleza kwamba mchango wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif katika Sekta ya Elimu umekuwa mfano wa kuigwa na Viongozi wengine hapa Nchini.

Mwalimu  Ussi Machano alisema kwamba mchango huo kwa kiasi kikubwa umeipunguzia mzigo mkubwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika     ukamilishaji wa Majengo mbali mbali ya Skuli yanayoanzishwa na wananchi wenyewe kwa mpango wa kujitolea.

Huu ni mkupuo wa Pili kwa Benki hiyo ya NMB kusaidia vikalio kwa Skuli za Donge na Kitope.

 

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

30/3/2014.

Baadhi ya Masheha wa Wilaya ya Mjini walioshiriki maadhimisho ya sherehe za kutimia Mwaka Mmoja wa Usajili wa Ardhi Zanzibar zilizofanyika katika Hoteli ya Bwawani ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Baadhi ya Masheha wa Wilaya ya Mjini walioshiriki maadhimisho ya sherehe za kutimia Mwaka Mmoja wa Usajili wa Ardhi Zanzibar zilizofanyika katika Hoteli ya Bwawani ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Balozi Seif akionyesha  Kadi Maalum za kusajili Ardhi kwenye sherehe za mwaka mmoja wa usajili wa Ardhi kadi ambayo itakuwa na uwezo kamili wa kumbu mbuku za muhusika katika utumiaji wa ardhi.

Balozi Seif akionyesha Kadi Maalum za kusajili Ardhi kwenye sherehe za mwaka mmoja wa usajili wa Ardhi kadi ambayo itakuwa na uwezo kamili wa kumbu mbuku za muhusika katika utumiaji wa ardhi.

SMZ KUNDAA SERA MPYA YA ARDHI

Balozi Seif akimkabidhi Kadi ya usajili wa Ardhi Bibi Mwanakheir Mohd Maktubu baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili wa ardhi anayoitumia katika sherehe za mwaka mmoja wa usajili wa Ardhi.

Balozi Seif akimkabidhi Kadi ya usajili wa Ardhi Bibi Mwanakheir Mohd Maktubu baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili wa ardhi anayoitumia katika sherehe za mwaka mmoja wa usajili wa Ardhi.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko katika matayarisho ya mwisho ya kuandaa Sera mpya ya Ardhi itakayozingatia hali halisi ya mahitaji na matumizi bora ya  Ardhi iliyopo Nchini kwa Maendeleo ya Kiuchumi.

Sera hiyo itakwenda sambamba na mageuzi makubwa ya kuendeleza sekta hiyo katika kupanga upya matumizi ya ardhi yote ya Zanzibar yanayoendana na matayarisho ya Mipango Miji  yanayoendelea.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika sherehe za kuadhimisha mwaka mmoja wa usajili wa Ardhi zilizofanyika katika Hoteli ya Bwawani  Mjini Zanzibar.

Balozi Seif alisema usajili wa ardhi Nchini kwa muda mrefu ulikuwa ukikatishwa mara kwa mara kutokana na migogoro ya ardhi inayoleta kero kutokana na mizozo ya Kijamii na kuigharimu Serikali Kuu fedha nyingi.

Alisema migogoro mingi iliyojichomoza katika maeneo mbali mbali hapa Nchini imekuwa ikisababishwa na baadhi ya Wananchi kwa kuamua kutumia ardhi kinyume na utaratibu uliowekwa  kisheria wa haki ya matumizi ya ardhi.

“ Usajili wa ardhi umekuwa ukihimizwa sana Duniani kutokana na kupelekea usimamizi mzuri wa matumizi ya ardhi. Usajili wa Ardhi unahitaji ardhi kutambuliwa, kupimwa na hatimae miji na vijiji vipangwe bila ya migogoro “. Alisisitiza Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na watendaji wa Taasisi za Ardhi na Upimaji  katika hatua za awali za utambuzi na upimaji hasa kwenye maeneo ambayo bado hayajafanyiwa usajili ili kufanikisha vizuri azma hiyo njema ya Serikali.

Alisisitiza kwamba kwa vile ardhi ni msingi mkuu wa maendeleo kwa nchi yoyote Duniani, Wananchi hawana budi kujenga katika maeneo yaliyopimwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa na sheria za mipango miji na vijiji.

“ Katika usajili wa ardhi malengo yaliyokusudiwa ni kuona kuwa watumiaji halali wa eneo husika wanatambuliwa na maeneo yanapimwa, vyenginevyo uvamizi wa ardhi na ujengaji holela usiofuata taratibu kamwe hautovumiliwa “. Alionya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Katika kufanikisha nia njema ya Taifa ya matumizi mazuri ya ardhi  Balozi Seif  alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inapanga upya matumizi ya ardhi katika ukanda wa pwani, Vijijini na tayari zoezi hilo limeshakamilika katika Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alieleza kuwa jitihada kubwa zimechukuliwa na Serikali juu ya suala zima la upimaji na usajili wa ardhi ambapo jaribio la kwanza  la usajili kwa utaratibu wa utambuzi unaoambatana na upimaji wa ardhi lilifanyika mwaka 1994 kwa ufadhili wa Serikali ya Finland kupitia mradi wa ZILEM.

Balozi Seif alifahamisha kwamba mipangilio ya upimaji wa mashamba kwa lengo la usajili ilianza kufikiriwa tokea mwaka 1920 lakini ilishindikana kutekelezwa kutokana na ukosefu wa fedha.

Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema mnamo mwaka 1981 Serikali ilifanikiwa kufanya upimaji wa ardhi kwa msaada wa Serikali ya Sweden lakini usajili wake haukufanyika.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliishukuru Serikali ya Finland kupitia Balozi wake aliyopo Nchini Tanzania pamoja na kuipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye zoezi hilo la usajili  wa ardhi kupitia mradi wa MKURABITA. Akitoa Taarifa ya usajili wa ardhi MrAJIS WA Ardhi Zanzibar Bibi Mwanamkaa Abdullrahman Mohd alisema Nyumba  zipatazo elfu 1,300 zimeshasajiliwa katika mshehia 16 zilizomo ndani ya Wilaya ya Mjini.

Bibi Mwanamkaa alisema wataalamu na watendaji wa Ofisi ya msajili wa ardhi wanaendelea kuyatambua mashamba yapatayo 22,746 Unguja na Pemba.

Alieleza kwamba katika kwenda sambamba na zoezi hilo la usajili wa ardhi hatua zinaendelea kuchukuliwa katika usajili wa ardhi kupitia mfumo wa kisasa wa mtandao wa Kompyuta.

Hata hivyo Mrajisi huyo wa Ardhi alielezea changamoto zilizojitokeza katika zoezi hilo la usajili wa ardhi katika maeneo yaliyokatwa eka tatu tatu ambayo mengi kati yao yamevamiwa kwa ujenzi wa nyumba za kudumu .

Aliipongeza Serikali Kuu kwa kusaidia utatuzi wa migogoro ya ardhi katika baadhi ya maeneo hapa nchini ambao umeleta  utulivu baina ya pande zinazojichomoza kuzozana katika matumizi ya ardhi hizo.

Mapema Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban alisema migogoro inayofanywa na wajanja katika matumizi ya ardhi inaweza kuondoka  iwapo wananchi wataamua kusajili ardhi wanazozitumia kila siku.

Waziri Shaaban alisema lengo lililowekwa na Ofisi ya Usajili wa Ardhi ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2015 usajili wa ardhi ufikie asilimia 50% ya ardhi yote ya Unguja na Pemba.

Alisema eneo lililosajiliwa hadi sasa bado ni dogo ikilinganishwa na ardhi yote iliyopo katika Visiwa vya Zanzibar. Hivyo juhudi za Wananchi katika kushirikiana na Serikali Kuu zinahitajika zaidi ili kufanikisha mpango huo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Katika Maadhimisho hayo ya kusherehekea mwaka Mmoja wa usajili wa Ardhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alizindua kadi ya usajili wa ardhi sambamba na kuzindua jarida la Ardhi.

Kadi hiyo yenye nambari maalum ya utambulisho na kumbu kumbu za usaliji wa ardhi itampa fursa muhusika kuitumia wakati wowote badala ya kuranda na waraka.

Ujumbe wa mwaka huu wa usajili wa ardhi Zanzibar ni Nyumba yangu imesajiliwa yako jee?

NA Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiongoza Mamia ya Wananchi  pamoja na Viongozi wa Serikali, Siasa na Dini wa Mji wa Dodoma na Vitongoji vyake katika Kuuaga Mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Mara Marehemu John Tuppa

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiongoza Mamia ya Wananchi pamoja na Viongozi wa Serikali, Siasa na Dini wa Mji wa Dodoma na Vitongoji vyake katika Kuuaga Mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Mara Marehemu John Tuppa

Mkurugenzi wa Mapinspaa Zanzibar Abeid Juma, akimueleza Maalim Seif hali ya usafi na uchafu katika soko la matunda Mombasa Zanzibar.

Mkurugenzi wa Mapinspaa Zanzibar Abeid Juma, akimueleza Maalim Seif hali ya usafi na uchafu katika soko la matunda Mombasa Zanzibar.