Naibu Katibu Mkuu UV-CCM, Zanzibar shaka Hamdu Shaka

Naibu Katibu Mkuu UV-CCM, Zanzibar shaka Hamdu Shaka

Umoja wa Vijana wa CCM umemtaka Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kuachia ngazi kama chama chake hakiafiki utendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC)kwa vile viongozi wa Tume hiyo pamoja nayeye wameteuliwa na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.

Ushauri huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kuwapongeza wananchi kwa ushindi wa CCM uliopatikana katika uchaguzi mdogo jimbo la Kiembesamaki.

Shaka amesema Tume ya Uchaguzi Zanzibar ni chombo cha kikatiba na kisheria ambapo viongozi  wake ni wateuliwa wa Rais ambao hupatikana baada ya Rais kushauriana na wasaidizi wake akiwemo Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad na Makamo wa Pili Balozi Seif Ali Idd.

Amesema kitendo cha Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF Omar Ali Shehe kutaka Tume na sekreterieti yakle iivunjwe kutokana na wao kupoteza imani na chombo hicho hakikuwa kitendo cha kiungwana katika uwajibikaji wa pamoja na kuheshimu msingi ya demokrasia chini ya Serikali ya Umoja wa Kiataifa Zanzibar.

Amesema kama CUF hamna imani na ZEC,Makamo wa kwanza wa Rais nae ajiuzulu,hata yeye ni sehemu ya uteuzi wa Rais hivyo hana haki ya kuwanyooshea kidole wenzake na kutaka wafutwe kazi”Alisema Shaka huku akishangiliwa,

Amesema iwapo CUF imejipima na kujiona haitafurukuta mwaka 2015 katiika uchaguzi mkuu wa Zanzibar wasiishie kulalamika na kutaka kususa ila wanachotakiwa sasa ni kumshauri Katibu Mkuu wa o ambaye ni Makamo wa Kwanza wa Rais akae chonjo katika siasa.

Alisema chama cha CUF ni kawaida kwao kuleta mbwembwe za kisiasa na kuwapaka matope watendaji dhamana wa ZEC tokea mwaka 1995 na mara zote huwa hawalalamikii matokeo ya uchaguzi huko Pemba na badala yake wakilalamika majimbo ya Unguja wakati ni ZEC ndiyo inayosimamia kazi yote ya kuratibu uchaguzi.

Shaka amesema tabia ya visingizio vyao vya madai ya  kutokewepo  kwa uchaguzi huru na wa haki Zanzaibar vimekuwa vikiwagharimu wananchi na kukumbusha matukio ya Januari 26 na 27 mwaka 2001 na kuwataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wasiokubali kushindwa katika uchaguzi wa vyama vingi.

Amesema waangalizi wa ndani na vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi mdogo wa Kiembesamaki wote walisema uchaguzi ule ulikuwa ni wa mfano lakini jambo la ajabu CUF wameendelea kulaumu ili kuwayumbisha wananchi wa Zanzibar.

“Maalim Seif nebda kawatake radhi viongozi wako waliokupandisha chati kisiasa,umewakosea kina mzee Aboud Jumbe na hayati Mzee Idris Abdul Wakil,nenda kaburi na kamuwahi Mzee Jumbe mdondokee,ikulu utaisikia kwenye radio na hutaweza kuingia kwa kuwa umewasaliti wenzako”Alisema Shaka.

Naibu huyo Katibu Mkuu wa UVCCM amewataka wabunge wa bunge la katiba kuongozwa na uzalendo katika kujadili rasimu ya pili ya katiba na kuhakikisha Taifa linabakli katika mikono salama chini ya misingi iliowekwa na waasisiwa Mungano Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.

Amesema wakumbuke kuwa sumu huwa haonjwi na ni makosa kufanya majaribio ya maisha ya watu kama wafanyavyo madaktari kwenye vyumba vya maabara huku akisema kuwa mfumo wa Muungano wa serilali mbili umelijenga Taifa katika amani,utulivu na usalama kwa miaka 50.

Kwa upande wake Mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo amewakabidhi watendaji wa CCM katika matawi matano ya jimbo hilo na kuwataka kuwa makini katika kufanikisha kazi zao za kila siku za kisiasa.

Mahmoud Alisema kwamba kazi ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi imeanza na atahakikisha yeye ni chama cha Mapinduzi wanatekeleza kwa vitendo hatua kwa hatua na kuwaletea maendeleo wananchi.

Alitoa jumla la pikipiki kumi zenye thamani ya shilingi milioni 20 katika matawi ya Kiembesamaki,Kisima Mbaazi,Mbweni,Chukwani na Buyu.

Advertisements