imagesPolisi mmoja ameuliwa na mwengine amejeruhiwa na watu wanaosadikiwa majambazi katika hoteli ya Pongwe Bay Resorts usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kusini Unguja Augostino Olomy amesema askari hao waliokuwa wakilinda kwa kushirikiana na walinzi wa hoteli walivamiwa na kundi la majambazi wenye silaha ya SMG.

Amesema majambazi hao idadi yao haijajulikana walifyatua risasi zilizowajeruhi askari hao na kuiba silaha iliyokuwa ikimilikiwa na mmoja wa askari hao.

Olomy amemtaja askari Koplo Mohammed Mjombo alijeruhiwa vibaya na kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu hospitali ya Mnazimmoja.

Amesema askari mwengine Ibrahim Juma aliejeruhiwa bega la kulia anaendelea na matibabu katika hospitali hiyo

Kamanda Olymi amesema majambazi hao waliiba simu ya mkononi na hakuna mgeni aliejeruhiwa.

Amesema hadi sasa jeshi la polisi linawashikilia watu watatu kwa mahojiano.

Hoteli ya Pongwe Beach Resorts ilioko  Mkoa wa Kusini Unguja inamilikiwa na raia wa Italia Suzan Marcov.

Advertisements