uamshoViongozi wa jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam(JUMIKI) wamefutiwa mashitaka na mahakama ya wilaya ya Mwanakwerekwe dhidi ya kesi ya kufanya mkusanyiko bila ya kibali iliofunguliwa Mei mwaka jana visiwani Zazibar.

Uamuzi huo umetolewa na Hakim Ame Msaraka Pinja baada ya kukamilika kusikilizwa kesi hiyo na washitakiwa kuonekana hawana hatia katika mamshitaka yaliokuwa yamefunguliwa na Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar DPP mapema Mei mwaka jana.

Hakimu Pinja amesema kwa kuzingatia mashahidi wanne upande wa mashitaka pamoja na washitakiwa wenyewe waliithbitishia mahakama kwamba katika mkusanyiko wao hawakuwa wakizungumzia mambo ya dini ispokuwa wakizungumzia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Ameswema kwa msingi huo wqashitakiwa hawakuhitaji kuwa na kibali chochote cha kisheria kabla ya kuandaa mkusanyiko huo kwa vile walikuwa wakizungumzia mambo ya Muungano na kwa msingi huo hakuna shitaka linalowatia hatiani na mahakama imetupilia mbalio dai hilo.

Amesema baada ya mahaka kupitia jalada la kesi hiyo,imeonekana washitakiwa hawana hatia,ninawaachia huru kwasababu kosa waliloshitakiwa halikuhitaji kibali cha mufti kabla ya kuandaa mkusanyiko huo”Alisema Hakimu Pinja.

Hata hivyo Hakimu huyoi wa mahakama ya wilaya ya Mwanakwerekwe alisema upande wa mashitaka wa Serikali kama haujaridhika na uamuzi wa mahakama hiyo unaweza kukata rufaa mahakama ya mkoa ndani ya siku 30 tangu kutolewa kwa uamuzi huo.

Washitakiwa katika kes\hi hiyo ni Farid Hadiy Ahmed Mussa Juma Issa, Haji Sadif Haji,Suleima Juma Suleiman,Fikirini Mjawaliwa Fikirini na Abdallah Said Ali. .

Washitakiwa walifunguliwa mashitaka kwa kufanya mihadhara ya kiislam bila kibali cha mufti kinyume cha kifungu cha 6(1)(2) cha kanuni za kuidhinisha na kuratibu mihadhara zinazotengenezwa chini ya kifungu 15(1) ya sheria Namba 9 ya mwaka 2001 ,kifungu cha 10(1)(c) na kifungu cha 14(2) ya sheria namba 9 ya mwaka 2001.

Ilidawa bila ya halali Mei 26 mwaka jana majira ya saa 3;30 huko katika viwanja vya Lumumba wilaya ya Mjini Unguja washitakaiwa walifanya mihadhara ya kiislam bila ya kuomba kibali cha mufti wa Zanzibar.

Advertisements