Na Juma Abdallah Ali.

Mfumo wa usikilizaji wa kesi mahakamani na hatimae kutoa hukumu unaonekana na mashaka yanayosababisha wananchi wanaonyimwa haki zao katika taasisi hizo kutokuwa na imani nazo.

Hatua hiyo inatokea hasa kesi inapochukua muda mwingi katika hatua za kutajwa, kusikilizwa, kuitwa mashahidi na hatimae kutolewa hukumu.

Kwa maoni yangu bado kumekuwa na mashaka katika utowaji wa  hukumu hasa kesi zinazohusu makosa ya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kutokana na baadhi ya sheria kupitwa na wakati.

Wanaharakati kutoka taasis za ndani na nje kupitia miradi mbali mbali wanaendelea kulipigania suala la ucheleweshaji wa kesi unaosababisha kutolewa hukumu zinazochangi kuendeleza vitendo hivyo.

Wanaharakati  kutoka chama cha wanadishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA na Jumuiya ya wanasheria wanawake Zanzibar ZAFELA ni miongoni mwa taasisi zinazoendesha miradi yenye lengo la kulipatia umfumbuzi tatizo hilo.

Taasisi hizo zinazoshirikiana kuendesha mradi wa kuwawezesha wanawake kiuchumi na usawa wa kijinsia GEWE zinaendeleza juhudi kuona kesi za unyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto zinaendeshwa kwa misingi ya haki na sheria.

Nina mfano mmoja wa kesi ya iliyotolewa hukumu kwa mtuhumiwa Nassour Kassim Chande mkaazi wa Muyuni aliempa ujauzito mtoto wa mke wake wa ndoa kuonekana hana hatia na kuachiliwa huru katika mahakama ya mkoa Mwera.

Kesi hiyo iliyochukua takriban miaka mitatu ni moja ya ucheleweshaji wa kesi unaolalamikiwa na wananchi pamoja na kuwavunja moyo  wanaojitolea kutoa ushahidi kesi za aina hiyo.

Mlalamikaji wa kesi hiyo iliyotolewa hukumu June 30 mwaka huu Nadhif Mwita ambae ni baba  mdogo wa mtoto aliepewa ujauzito amesema uwamuzi huo sio mwisho wa kusitisha harakati zake za kupambana na vitendo vya udhalishaji wa kijinsia dhidi ya wanakwake na watoto.

Akizungumza na mwandhisi wa makala hii amesema kutokana na sababu zilizotolewa mahakamani hapo za kumwachia huru Nassour hajaridhika nazo na anatarajia kukata rufaa kwenye mahakama kuu.

Amesema madai ya mahakama kuwasilikiza mashahidi watano upande wa mlalamikaji ukiwemo ushahidi wa daktari haukuweza kumtia hatiani mtuhumiwa huyo hakubaliani nayo.

Nadhifu amesema kesi kama hizo zinapotokea zinakuwa na siri kubwa na hakimu alipaswa kutumia akili pamoja na kuwepo sheria.

’’Baba yake mzazi huyu mtoto ni mlemavu haoni hawezi kushuhgulikia pilika za mahakamani….mimi mlalamikaji sijaridhika nitakwenda mbele zaidi kwa kukata rufaa niende mahakama kuu’’. Alisema Nadhif.

Hata hivyo Nadhif ameiomba serikali kuwa makini katika mapambano dhidi ya vitendo vya unyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kwa kile alichodai kesi kama hizo hatofungwa mtu.

Hivi karibuni akizungumza na wandishi wa habari wanafuatilia vitendo vya udhalishaji wa kijinsia Mkurugenzi mkuu wa mashtaka Zanziba DPP Ibrahim Mzee  ametaja miongoni mwa ushahidi unaokataliwa mahakaman ni uvumi au maneno ya kusikia.

Amesema ushahidi unaotakiwa ni wa moja kwa moja wa kuona tukio au mazingiara yaliofanyika tukio hilo.

Mzee amefahamisha ushahidi mwengine unaoweza kupokelewa ni wa kitaalamu ukiwemo maelezo ya daktari  na kipimo cha vinasaba ‘DNA’ hatua hiyo inayochangia kuchelewa kwa kesi kutolewa hukumu.

‘’ Kuna suala la mishine ya DNA lakini Zanzibar hatuna pengine ingekuwepo kesi kwa kiwango kikubwa zingendeshwa haraka kwa sababu kama hakuna alieona, lakini mtoto akatolewa uchafu katika sehemu za siri tungeona ‘particles’ za yule mwanamme’’. Alitoa mfano Mzee.

Hata hivyo amesema sheria ya ushahidi sura ya tano ndio inayongoza ushahidi unaopokolewa mahakamani na sio kila ushahidi unaokusanywa na jeshi la polisi unaweza kupokewa.

Akinukuku sheria ya ushahidi aliyoitaja ya zamani ya mwaka 1917 ndio inayoweka utaratibu wote kama ushahidi huo unaweza kupokolewa au kutupwa na mahakama.

Afisa dhamana wa mahakama kuu na mkoa Unguja Raya Suleiman amesema undeshaji wa kesi za udhalilishaji wa kijinsia ni mkubwa kutokana na ugumu wa upelelezi, wa kupata ushahidi unaohitajika.

Hata Raya amekiri kesi mahakamani kuchukua muda mrefu wakusikilizwa na  kutokana na kukosa ushahidi na kuifanya mahakama kumwachilia huru mtuhumiwa.

Amesema hali hiyo inatokana na ukosefu wa waendesha mashtaka wenye utaalamu uliobebea.

‘’ Tumepata maombi mengi ya kufuta kesi kutokana na hali hiyo ikiwemo familia kuoneana muhali mtu anaweza asichukue pesa lakini akiona ah! ndo nimpeleke jamaa yangu ah! siendi’’. Alisema Raya.

Amesema hali kama hiyo kesi haiwezi kuendelea hata iwe nzuri na mwelekeo wa kumtia hatiani mtuhumiwa na nyingi ya kesi kama hizo ni zile zenye mwelekeo wa kushinda.

Hata hivyo afisa huyo amewataka wandishi wa habari kuendeleza wajibu wao wa kuzifuatilia kesi za unyanyasaji wa kijinsia  kuzifichua na kuandika na kuripoti ili kuwasaidia watendaji kutimiza wajibu wao.

Afisa wa dawati la jinsia la watoto jeshi la Polisi  mkoa wa Kusini Unguja Sajenti Haji Mohammed Iddi amesema baadhi ya    ucheleweshaji kesi mahakamani unachangiwa na wazazi kwa kukaa zaidi ya wiki moja kuziripoti kesi za udhalilishaji wa kijinsia mahakamani.

Akizungumza na makala hii amesema wanapoziwasilisha kesi hizo mahakamani mambo mengi yanakosekana ikiwemo vielelezo vya mbegu za kiume kwa wathirika waliofanyiwa vitendo vya ubakaji.

Sajenti Iddi amesema wananchi mara nyingi wanalitupia lawama jeshi la polisi licha ya kutoa taalauma   lakini wanashindwa kufahamu jinsi ya kutunza ushahidi unaohitajika mahakamani wa kuendeshea kesi.

‘’Wanapotuletea sisi sasa na tunaanza moja na tunashindwa kufikia lengo kwa sababu mambo meng washavuruga kule mitaani…wanasahau kama kuna utaratibu hadi kufika jalada kule mahakamani’’. Alisema Sajenti huyo wa polisi.

Hata hivyo watendaji wa dawati hilo wamesema nao pia wanathirika na tatizo la ucheleweshaji wa kesi za udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya watoto kutokanana na kuvunjika moyo mashahidi wanaotakiwa kwenda kutoa ushahidi mahakamni.

Aidha amesema madaktari nao pia wanachangia kuchelewesha   kesi mahamakni  kwa kushndindwa kutoa ushahidi mahakamani kunakosababisha kuchelewa kesi hizo.

‘’Suluhisho la matatizo hayo naimba mahakama mashahidi wetu wanapokwenda kutoa ushahidi mahakamani wasikilizwe…na kama kuna uwezekano tuongezewe mahakimu ili kesi zetu ziende haraka haraka…zisikae kwa muda mrefu kwa sababu inapokaa kwa muda mrefu hata yule shahidi ukimwita basi hajui hata anachokisema’’.Alitoa ombi  hilo Sajenti Iddi wakati akihojiwa na mwandishi wa makala hii.

Dawati hilo pia limesema kipimo cha DNA kwa sasa kimekuwa na usumbufu kutokana kuwepo kimoja kwa Tanzania nzima, hivyo zinapopelekwa kesi zinakaa kiasi ya mwaka mmoja bila ya majibu.

Sajenti Iddi amesema kwa mwezi kiasi ya kesi tatu au nne zinahitaji kufanyiwa vipimo vy a DNA katika mkoa wa Kusini Unguja unaodaiwa kuwepo vitendo vingi vya udhalilishaji.

‘’Sasa hivi hata wahalifu wenyewe wamejijengea kwamba nikishafanya… ndo basi tena DNA yenyewe haipo unakaa tena mwaka mzima unasubiri DNA hamna kwa hivyo matukio yanazidi….kama tutakuwa na DNA yetu wenyewe hapa Zanzibar basi tukipata mifano kesi mbili tatu tu basi inawezekana kesi za udhalishaji kupungua kwa kasi’’ Alitanabahsha Sajenti huyo.

Nae afisa kutoka ZAFELA Jamila Mahamoud amesema katiba ya Zanzibar inaruhusu kuwepo na sheria zitakazondoa vitendo vya unyasaji wa kijinsia nyingi zao hazitoi nafasi hiyo kutokana na kupitwa na wakati.

Amesema sheria nyingi za muda mrefu hazilingani na wakati wa sasa kutokana na kuongezeka kwa aina ya makosa na wananchi hawazifahamu.

Jamila amesema katika utafiti mdogo walioufanya kupitia mradi wa GEWE wametoa mapendekezo ya kufanyiwa marekebisho kwa sheria hizo, lakini bado zinaendelea kutumia.

Amesema watu wengi wanalalamikia utekelezaji wa sheria hizo licha ya kufahamu taratibu za kutunza ushahidi hasa vitendo vya unyasaji wa kijinsia, lakini wanapokwenda mahakamani wanakwazwa.

Ametoa mfano wa sheria ya ushahidi inayosema hakimu ajiridhishe bila ya chembe ya kuwepo shaka, akisema huo ni upungufu mkubwa wa sheria unaotoa nafasi kwa mahakama kuwachia huru watuhumiwa.

‘’ Kila mmoja sote tunajua masuala ya udhalilishaji hasa huu wa ‘kingono’ unafanyika ukiwa katika hali ya usiri na kuonekana inakuwa kwa bahati nzuri sana’’ Alisema Jamila.

Sheria ya ushahidi ya mwaka 1917 na ile ya  makosa ya jinani inahitaji kufanyiwa marekebisho ili kupunguza ucheleweshaji wa kesi mahakamni pamoja na kusaidia kukomesha vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

 

 

 

Advertisements