Archive for August, 2014

SMZ YAPIGA MARUFUKU BAA

Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk,akizungumza na wananchi na wamiliki wa mahoteli na baa katika kijiji cha Kiwengwa mara baada ya ziara yake ya kutembelea hoteli hizo

Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk,akizungumza na wananchi na wamiliki wa mahoteli na baa katika kijiji cha Kiwengwa mara baada ya ziara yake ya kutembelea hoteli hizo

Waziri wa Habari,Utamaduni , Utalii na Michezo Saidi Ali Mbaruok amepiga marufuku shughuli zote za upigaji wa disko katika eneo la kiwengwa mpaka pale Serikali ya wilaya itapo toa maelekezo maalumu ya upigaji wa disko hilo kwa utaratibu unao faa.

Agizo hilo amelitoa leo huko kiwengwa Mkoa wa kaskazini “A”wilaya ya kaskazini B Unguja katika Ofisi ya umoja wa maendeleo wa kijiji cha kiwengwa wakati alipokuwa akifanya mazungumzo na wamiliki wa mabaa mikahawa,na kumbi na starehe juu ya kukithiri wa upigaji wa magoma kucha.

Amesema amelazimika kuzifunga shughuli zote za upigaji wa madisko usiku kutokana na kutokua na  utaratibu mzuri wa upigaji ngoma hizo usiku  haliambayo inapelekea wageni wa kitalii na wenyeji kuchukia hali hiyo kwa kukosa usingizi na kusumbuliwa wagonjwa wenye shindikizo la damu.

Amsema hali hiyo haiwezekani kuona inaendelea katika hali kama hiyo kwani inapoteza muelekeo na mstakabali mwema wanchi na  raia kwaujumla.

 “Nimepokea messsege ya kwamba watalii wamefika kusema wanaondoka na kutafutiwa sehemu nyengine wakapunzike kutokana na zogo kuwa jingi la madisko,hili hiliwezekani liendelee”lisema Waziri.

Aidha alisema haiwezekani kuona utamaduni wa burudani unavurugwa kituambacho ni kosa kufanya hivyo na kwenda kinyume na taratibuzao selka zao.

“kuazia leo napiga marufuku mpaka sheha wa shehia hii aridhie hata kama kuna kibali ,kwani sheha yeye ndio anae jua hali za raia wake kuna wagonja,na wenyemaradhi ya kuhitaji kupumzika hatutaki kuona masuala yasio na utaratibu.”aliongeza Waziri.

 “mimi kazi yangu ni kuutangaza utalii nasio utalii uharibiwe ,tufahamu kua ulalii Zanzibar ndio uchumi unao tegemewa kwa sasa kwa hivyo tulinde,”aliongeza Waziri Said.

Hata hivyo waziri huyo alichukia vitendo vya uwasharati vilivyo tapakaa katika kijiji hicho na kujenga mabaa karibu na nyumba za ibada kitu ambacho aliagiza kwa mkuu wa wilaya kuyafanyia kazi.

Nao wazazi wa kiwengwa Othumani mnyanja na mtumwa Rashidi walisema kiwengwa hivisasa imepoteza muelekeo kwani watoto wao wanaishia katika madisko na kukosa masoma kitiambacho ni hatari kwao.

Aidha walisema kua watoto wao wakiwa na umri mdogo na kujishughulisha na masuala ya kimapezi jambo linalo wafanya nialama ya kupotea na kuacha mila za kislamu.

Wakitaja maeneo ya nayopigwa miziki na watoto wao kwenda ni pamoja na  maeneo yanayo pigwa madisko hayo ni pamoja na ,kigorofani, vishani wazalendo pub, Kamili View,Obama Baa na kigorofani eneo la mafarasi.

 Nae miliki wa ukumbi wa Disko wa PERUU B, Peruce Osward Buhoma  akiulizwa swali na waziri kwanini anafanya mazogo usiku alikiri kwa kusema hufanya hivyo kwaajili ya kuvuta wateja na kufanya ushindani kila mmoja kwajili ya  kusikika zaidi kuliko mweziwe.

Bibbi huyo na wezake walisema wanaweza kujirekebisha lakini pawe na utaratibu wa kupiga madisko kwa zamu na utaratubu mzuri utakao wekwa na uongozi

Advertisements

DR. SHEIN AKUTANA NA DIASPORA

SHEIN 2SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini mafanikio makubwa yalioanza kupatikana kutoka kwa Wazanzibari wanaoishi nchi za nje (Diaspora) na ndio maana ina mpango maalum wa kuandaa Sera na hatimae Sheria kwa lengo la kuendeleza zaidi mafanikio hayo.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein, aliyasema hayo leo mara baada ya chakula maalum cha mchana alichowandalia Wazanzibari wananoishi nchi za nje (Diaspora) huko katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.

 

Katika ghafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mawaziri, Wawakilishi, Wabunge Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Makatibu Wakuu na viongozi wengine.

 

Wazanzibari wanaoishi nchi za nje waliojumuika katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Dk. Shein ambao wapo hapa nchini kwa mapumziko ni kutoka nchi mbali mbali zikiwemo Uingereza, Canada, Marekani, Denmark, Sweden, Oman, UAE, Ujerumani, Uholanzi, Austria, Switzerland.

 

Akitoa nasaha zake mara baada ya chakula hicho cha mchana alichowaandalia Wazanzibari hao, Dk. Shein alieleza kuwa michango na misaada yao imeanza kitambo kwa kuweza kusaidia nyenzo pamoja na vifaa mbali mbali hapa nchini na kuzitaja nchi kadhaa ambazo tayari zimeshapata mafanikio kutoka kwa wananchi wake waishio nchi za nje.

 

Alieleza kuwa mbali ya vifaa na nyenzo hizo mbali mbali Wanadiaspora hao pia wameweza kuchangia utaalamu wao walionao ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuendeleza sekta ya elimu hapa nchini kupitia Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kwa kuweza kufundisha elimu ya Shahada ya Uzamivu.

 

Dk. Shein alieleza kuwa wataalamu hao wameweza kutoa utaalamu wao kwa Shahada hiyo ya Uzamivu katika lugha ya Kiswahili na tayari hivi sasa wanafunzi wanaowafundisha wanaendelea na masomo yao vizuri. Ambapo pia wapo wengine waliojitokeza kuonesha uzoefu wao wa kazi.

 

Alisisitiza kuwa nia na lengo la Serikali ni kufanya vizuri zaidi kwani ishara ya mafanikio imeshajitokeza kwa hivi sasa na kusisitiza kuwa kila Mzanzibari alieko nje na ndani ya Zanzibar ana fursa na nafasi ya kuijenga nchi yake. Pia,alieleza kuwa mchakato huo wa kuanzisha Diaspora wa Tanzania wakiwemo kutoka Zanzibar aliuanza yeye na Rais Jakaya Mrisho Kikwete tokea akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutambua umuhimu wake.

 

Aidha, Dk. Shein aliwataka Wanadiaspora kuendeleza misingi ya amani na utulivu kwani ni kawaida ya Wazanzibari wakiishi nchi za nje huwa hawabadilishi hulka wala desturi zao hatua ambayo imewajengea sifa kubwa. “Zanzibar inasifika sana kwa amani na utulivu”,alisema Dk. Shein

 

Sambamba na hayo, Dk. Shein alieleza kuwa Zanzibar imeweza kupata mafanikio makubwa hasa katika sekta ya utalii ambayo hivi sasa imeweza kutangazwa zaidi katika vyombo vya habari mbali mbali duniani ikiwemo BBC kwa kutambua kuwa Zanzibar ni waasisi wa sekta hiyo na ina vivutio na sifa nyingi za utalii.

 

Mapema Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa, Uwekezaji na Uchumi Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa alieleza kuwa nchi nyingi duniani zile zinazopokea Diaspora na zile zinazozalisha Diaspora zimepatambua umuhimu na mchango wa Diaspora katika maendeleo ya Kijamii na kiuchumi ambapo kwa upnde wa Zanzibar tayari faida imeshaanza kupatikana hususan katika sekta ya afya na Elimu.

 

Alieleza kuwa Ofisi inayoshughulikia masuala ya Diaspora imekuwa ikifanya juhudi kubwa ya kuwa karibu na Diaspora na wengi wao tayari wameshuhudia kwa macho yao juhudi hizo na kadiri siku zinavyokwenda mbele mashirikiano baina ya ofisi hiyo yamekuwa yakiongezeka.

 

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Wanadiaspora Bi Hafsa Hassan Bamba walitoa shukrani zao kwa mwaliko huo na kutoa pongezi kwa jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Mheshimiwa Rais ya kuwashirikisha kikamilifu katika harakati za maendeleo ya nchi yao.

 

‘Sisi Wanadiaspora hatuna cha kukulipa kwa jitihada za maendeleo ya nchi yetu. Bila shaka Mwenyezi Mungu ndiye atakaekulipa kwa jitihada hizi na tunaomba dua akuzidishie mapenzi uliyonayo ya kuwa karibu nasi kwa kila uchao” alisema Bamba.

 

Wanadispora hao, waliahidi kuwa Mabalozi na Mawakala kwa kuitangaza Zanzibar katika sekta zote za maendeleo na kijamii na kuiomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuoneza juhudi katika kukamilisha mchakato wa kuandaa Sera na Diapora kwa lengo la kuimarisha maendeleo na maslahi ya Wazanzibari waishio nchi za nje.

 

Katika hafla hiyo kikundi cha taarabu cha JKU kiliweza kutoa burudani safi kwa waalikwa wote pamoja na viongozi ambapo Dk. Shein katika nasaha zake alikipongeza kikundi hicho kwa kutoa burudani safi ikiwa ni pamoja na kutoa burudani ya nyimbo za asili zilizoibwa na waimbaji mahiri wa taarabu asilia hapa nchini.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Bi Hafsa Hassan Mbamba kwa niaba ya Wazanzibari wanaoishi  Nchi za nje  (Diaspora) akitoa neno la  shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein   kwa mwaliko huo na kutoa pongezi kwa jitihada zinazo chukuliwa na Mheshimiwa Rais na Serikali yake kwa ujumla,baada ya hafla ya chakula katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.

Bi Hafsa Hassan Mbamba kwa niaba ya Wazanzibari wanaoishi Nchi za nje (Diaspora) akitoa neno la shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa mwaliko huo na kutoa pongezi kwa jitihada zinazo chukuliwa na Mheshimiwa Rais na Serikali yake kwa ujumla,baada ya hafla ya chakula katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.

SHEIN 10

Baadhi ya Wazanzibari wanaoishi  Nchi za nje  (Diaspora) wakiwa katika chakula walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar

Baadhi ya Wazanzibari wanaoishi Nchi za nje (Diaspora) wakiwa katika chakula walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar

 Wazanzibari wanaoishi nje ya Nchi (Diaspora) wakichukua chakula walichoaandaliwa na   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.[

Wazanzibari wanaoishi nje ya Nchi (Diaspora) wakichukua chakula walichoaandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar.[

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika hafla ya chakula alichowaandalia  Wazanzibari wanaoishi Nchi za nje  (Diaspora)  katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika hafla ya chakula alichowaandalia Wazanzibari wanaoishi Nchi za nje (Diaspora) katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar leo

MANSOUR YUSSUF HIMID AKUTWA NA KIWANGO KIKUBWA CHA RISASI

Mansour Yussuf Himid

Mansour Yussuf Himid

Jeshi la polisi Zanzibar linamchunguza aliekuwa waziri wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mansour Yussuf Himid baada ya kukutwa na kiwango kikubwa cha risasi kinyume na sheria nyumbani kwake Chukwani.

Himid kwa hivi sasa anashikiliwa na jeshi hilo alikutwa na risasi 519 zikiwemo 112 za silaha aina ya Shot gun na 265 za bastola.

Jeshi hilo limesema linaendelea na upelelezi kujua sababu ya kiongozi huyo wa zamani kumiliki kiwango hicho cha silaha.

Naibu mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai Salum Msangi amesema Himid sheria za Zanzibar zinaruhusu mtu kumiliki risasi 50 za silaha ya shot gun na 25 kwa bastola.

Hata hivyo Msangi amesema Himid alikutwa na silaha ya Shot gun na bastola ya Barot anazozimiliki kihalali.

Aidha amesema kosa linalomkabili mtuhumiwa huyo ni kukutwa na kiwango kikubwa cha risasi kinyume na sheria.

Himid alieokosa sifa za kuwa mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki baada ya kuvuliwa uanachama wa CCM aliwahi kushika nyadhifa za ngazi za uwaziri.