Mansour Yussuf Himid

Mansour Yussuf Himid

Jeshi la polisi Zanzibar linamchunguza aliekuwa waziri wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mansour Yussuf Himid baada ya kukutwa na kiwango kikubwa cha risasi kinyume na sheria nyumbani kwake Chukwani.

Himid kwa hivi sasa anashikiliwa na jeshi hilo alikutwa na risasi 519 zikiwemo 112 za silaha aina ya Shot gun na 265 za bastola.

Jeshi hilo limesema linaendelea na upelelezi kujua sababu ya kiongozi huyo wa zamani kumiliki kiwango hicho cha silaha.

Naibu mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai Salum Msangi amesema Himid sheria za Zanzibar zinaruhusu mtu kumiliki risasi 50 za silaha ya shot gun na 25 kwa bastola.

Hata hivyo Msangi amesema Himid alikutwa na silaha ya Shot gun na bastola ya Barot anazozimiliki kihalali.

Aidha amesema kosa linalomkabili mtuhumiwa huyo ni kukutwa na kiwango kikubwa cha risasi kinyume na sheria.

Himid alieokosa sifa za kuwa mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki baada ya kuvuliwa uanachama wa CCM aliwahi kushika nyadhifa za ngazi za uwaziri.

Advertisements