Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Kibiashara cha Kimataifa Internationali Trade Center ICT Bibi Arancha Gonzalez walipokutana kwa mazungumzo jana wakati vikao mbali mbali vya Mkutano wa Nchi za Visiwa ukiendelea katika Mji wa Samoa katika ukumbi wa Mikutano wa Apia,[Picha na Ramadhan Othman,Samoa.]

Kituo cha Kimataifa cha Biashara (ITC) kimesema kiko tayari kuisaidia Zanzibar kutekeleza mkakati wake wa kuongeza ajira kwa vijana na kinamama kwa kutumia rasilimali zilizopo Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho chenye makao yake makuu mjini Geneva Uswizi, Bibi Arancha Gonzalez alieleza hayo jana wakati alipokutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein mjini hapa.   

Bibi Gonzalez alibainisha kuwa kisiwa kama Zanzibar ambacho hakina rasilimali kubwa ya ardhi mauzo ya mazao yake ya kilimo hayana budi kufanyika yakiwa yameongezwa thamani.

“suala muhimu la kuzingatia ni namna gani nchi za visiwa kama Zanzibar zin

aweza kupata maendeleo kwa kutumia rasilimali zake zenyewe iwe ni kilimo au utalii” alieleza Bibi Gonzalez.

Kwa hivyo alimueleza Mheshimiwa Rais kuwa suala kubwa la kuzingatia kwa Zanzibar ni kuongeza thamani ya mazao yake kama viungo kwa kuongeza ubora na kuvipa hadhi ya pekee (branding).

Kwa upande mwingine alieleza kuwa azma ya taasisi yake ni kusaidia kuimarisha miradi midogomidogo na ya ngazi ya kati ya vijana na wanawake hivyo kuongeza ajira ili kupunguza tatizo la ajira na umasikini katika jamii.

Mkurugenzi Mtendaji huyo alimueleza Mheshimiwa Rais kuwa Taasisi yake itashirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhakikisha kuwa inakuwa na mpango utakaowahusisha vijana wengi katika sekta ya utalii kwa maana ya ajira na kubuni shughuli zinazohusiana na sekta hiyo

Advertisements