Watu 39 wamefariki dunia papo hapo na wengine zaidi ya 86 kujeruhiwa vibaya baada ya mabasi mawili ya abiria kugongana uso kwa uso mkoani Mara.

ajali ya gari Ajali hiyo imehusisha Basi la Kampuni ya J4 Express lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari mkoani Mara, baada ya kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Mwanza Coach eneo la Sabasaba, mjini Musoma.

 Kwa mujibu wa chanzo cha habari katika eneo la ajali imetokea baada ya basi la J4 Express likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano karibu na eneo lenye daraja jembamba na kugongana basi jingine.

Gari hilo dogo liliingia mtoni na watu wawili kati ya watatu waliokuwepo walipoteza maisha.

Mkuu wa wilaya ya Butiama Katherina Mabula amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi huku mabasi hayo yakienda kwa mwendo wa kasi kwenye mteremko

Miongoni mwa watu waliokufa kwenye ajali hiyo ni madereva wawili wa mabasi hayo.                               

Advertisements