Archive for October, 2014

UGOMVI WA UVUVI CHWAKA, MARUMBI WAIBUKA UPYA

Rais wa Zanzibar akizungumzana wananchi wa vijji vya Chwaka na Marumbi Wilaya ya Kati

Rais wa Zanzibar akizungumzana wananchi wa vijji vya Chwaka na Marumbi Wilaya ya Kati

Ugomvi wa wavuvi wa kijiji cha Chwaka na Marumbi umeripotiwa kurejea tena licha ya serikali kuu kuchukua juhudi za kuwapatanishi.

Akizungumza na zenji fm radio kamanda wa polisi wa mkoa Kusini Unguja Juma Saad amesema usiku wa kuamkia jana wavuvi wa kijiji cha Marumbi waliwavamia wavuvi wa Chwaka na kuchukua mitegeo yao.

Amesema katika tukio hilo mvuvi mmoja wa Chwaka amejeruhiwa kwa kupigwa mawe pamoja na kuchukuliwa nyavu zao na mashine hors power 15 vifaa vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5.

Kamanda Saad amesema jeshi limefungua mashtaka na kumtafuta mtu anaedaiwa kumpiga jiwe mvuvi wa Chwaka……

Nae Sheha wa Shehia ya Chwaka Simai Msaraka Pinja akizungumza na mwandishi wetu amesema kurejea kwa ugomvi huo ni kinyume na makubaliano yaliofikiwa mbele ya rais wa Zanzibar.

Pinja ameiomba serikali kingilia kati kwa kuzuka tena mgogoro huo ulipatiwa ufumbuzi kwa kuwapatanisha wavuvi wa vijiji hivyo na kuweka mikapa ya maeneo ya uvuvi na hifadhi..

Wavuvi hao waliojeruhiwa Kassim Banzi Mgongo na Mwinyi Mwaka wamesema walivamiwa na wavuvi hao wakitumia faiba mbIli na kuchukua vifaa vyao vya uvuvi.

Wamesema hilo ni tukio la pili ndani ya kipindi cha wiki mbili cha kuvamiwa  na wavuvi wa Marumbi na kuchukua mitego yao…….

Ugomvi wa wavuvi wa vijiji vya Chwaka na Marumbi uliodumu kwa miaka mingi ulipatiwa ufumbuzi kiasi ya miaka miwili iliyopita na viongozi wa serikali akiwemo rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein kwa wavuvi kupatanishwa na kulipwa fidia za vifaa vyao vilivyoharibiwa.

20

Advertisements

Mahujaji 130 wamefariki dunia katika ibada ya Hija

iranSerikali ya Saudi Arabia imetangaza kuwa, mahujaji wasiopungua 130 wengi wao kutoka nchi za Kiarabu, wamefariki dunia wakati wa ibada ya Hija mwaka huu.
Taarifa zinasema kuwa, vifo vya idadi kubwa ya mahujaji vimesababishwa na umri mkubwa na maradhi. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, idadi kubwa ya Mahujaji waliofariki dunia ni kutoka Misri ambapo mahujaji 14 wameripotiwa kufariki dunia. Nchi nyingine ambazo mahujaji wao wamefariki dunia ni Iraq, Algeria, Sudan, Morocco, Somalia, Jordan na Mauritania. Imeelezwa kuwa, mahujaji wengine 213 wamelazwa kwenye hospitali za Saudi Arabia wakipatiwa matibabu kutokana na maradhi ya aina mbalimbali.
Hija inahesabiwa kuwa ni moja kati ya nguzo muhimu za dini tukufu ya Kiislamu, na Waislamu wenye uwezo wa kifedha na kiafya kutoka pembe mbalimbali duniani hushiriki kwenye ibada hiyo tukufu katika mji wa Makka. Mwaka huu, zaidi ya mahujaji milioni mbili walishiriki kwenye ibada hiyo ya kimaanaw

DUNIA INAKABILWA NA MATATIZO ATHARI ZA BINADAMU

sheinRais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amesema bado dunia inakabiliwa na matatizo yatokanayo na   kukithiri athari zitokanazo na binadamu  na matukio ya vimbunga,mateteko ya ardhi, volcano  na mabadiliko ya tabia nchi .

Dk Sheina ameyasema hayo jana kwenye baraza la Idd El Haj lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Kiisalam wilaya ya  Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Alisema matatizo hayo kwa namna kubwa yameleta athari  na hasara ya  kupoteza maisha ya watu na mali zao ikiwamo maafa yatokanayo na maradhi thakili  na hatari ya Ukimwi na ebola.

“Nchi yetu inaendelea kukumbwa na maafa mbalimbali ikiwemo ajali za barabarani, athari za mabadiliko ya tabia nchi na maeneo ya kilimo kuvamiwa na maji ya bahar,  visima vya asili kuingiliwa na maji chumvi”Alisema Dk Shein

Alisema hadi sasa jumla ya maeneo 145 yameathirika visiwani Zanzibar kwa kuingia maji  chumvi na kati ya maeno hayo  123 yapo kisiwani Pemba.

Dk Shein ameklitaja tatizo jingine ni kupanda  kina cha maji ya bahari duniani kwa maeneo yalioo chini ya mita tano kutoka usawa wa bahari na kueleza kuwa maeneo hayo yapo  kwenye hatari ya kuathirika zaidi kutokana na kukumbwa na hali hiyo.

Alisema maeneo ya aina hiyo kisiwani Pemba yana ukubwa wa mita za mraba 286 na yanakaliwa kwa  asiliamia 54 ya watu na kwa upande wa Unguja yana ukubwa wa mita za mraba 328 yakikaliwa na asilimia 29 ya maakazi ya watu.

“Baadhi ya wakati mvua huchelewa kunyesha , zinapokuja kiwango chake hupungua au hunyesha kwa kiwango kikubwa , upepo unapovuma  hautabiriki huku  pepo za kusi na kaksiakazi huvuma tofauti na viwango vilivyozioelekeka” Alisema Dk Shein.

Aidha alizungumzia hatari ya uchafuzi wa mazingira na kusema yanasibabishwa na binadamu kutokana na utupaji  taka hovyo ,bidhaa chakavu za kemika,  mifuko ya plastiki,uchimbaji wa mchanga na mawe ambapo maradhara yake huwa makubbwa na kutaka sheria  zisimamiwe vizuri hatari hiyo.

Rais huyo wa Zanzivar alisema sasa  hakuna budi zaidi ya kuchukua hatua madhubuti kwa mujibu wa sheria ikiwemo kuzuiia ujenzi kwenye vyanzoi vya maji na kwenye mabonde yaliotengwa kwa shughuli za kilimo.

Hata hivyo alisema Serikali zote mbili kwa kushirikiana na jumuiya ya kimataifa na washirika wa maendeleo watafanya jitihada ya kutekeleza mipango ya kitaifa na kimataifa katika kukabiliaana na maafa hayo.

“Masuala ya mazingira na tabia nchi yanayosibabisha maafa na majanga katika nchi yetu yanatekelezwa kwa kuzingatia sera na mipango ilioandaliwa’ Alisisittiza Dk Shein.

Kadhalika Rais Dk Shein aliwahimiza  waislama na wasiokuwa waislam nchini kuendelea kuthamini misingi ya amani,utulivu na upendo miongoni mwao bila ya kufarakana ,kutengana na kubaguana.

Katika hafla hiyo ya baraza la Eid  el Haj ilihudhiuriwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seeif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Naibu Kadhi Mkuu Mahmaoud Ngwali,  na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pande Ameir Kificho,

Wengine ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Makungu , Mke wa Rais  wa Zanzibar Mwanmwema Shein,Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Asha Suleima Idd na aliyekuwa Mke wa Rais wa kwanza  wa Rais  Zanzibar Mama Fatma Karume

Mamilioni ya Mahujaji wasimama Arafa

c96b50305f7e300bf2387f426d11ea43_LMahujaji zaidi ya milioni mbili wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu leo wamesimama katika uwanja wa Arafa kutekeleza nguzo kuu ya ibada ya Hija ambako wameshinda wakiomba dua na kumtaradhia Mola Muumba. Wageni hao wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu walishinda katika uwanja huo na wamenza kuondoka hapo baada ya kuzama jua wakielekea Muzdalifa.
Ripoti zinasema kuwa hadi jioni ya leo hakukuripotiwa tukio lolote la kutia wasiwasi.
Mahujai hao watakesha Muzdalifa na kumdakia Mina katika siku ya kumi ya Dhulhaji kwa ajili ya ibada ya kumpiga mawe shetani na kuchinja mnyanya wa sadaka.
Serikali ya Saudi Arabia inasema kuwa karibu Waislamu milioni moja na nusu kutoka nje ya nchi wanatekeleza ibada ya Hija mwaka huu mbali ya mamia ya maelfu ya Mahujaji kutoka maeneo mbalimbali ya Saudia kwenyewe