Rais wa Zanzibar akizungumzana wananchi wa vijji vya Chwaka na Marumbi Wilaya ya Kati

Rais wa Zanzibar akizungumzana wananchi wa vijji vya Chwaka na Marumbi Wilaya ya Kati

Ugomvi wa wavuvi wa kijiji cha Chwaka na Marumbi umeripotiwa kurejea tena licha ya serikali kuu kuchukua juhudi za kuwapatanishi.

Akizungumza na zenji fm radio kamanda wa polisi wa mkoa Kusini Unguja Juma Saad amesema usiku wa kuamkia jana wavuvi wa kijiji cha Marumbi waliwavamia wavuvi wa Chwaka na kuchukua mitegeo yao.

Amesema katika tukio hilo mvuvi mmoja wa Chwaka amejeruhiwa kwa kupigwa mawe pamoja na kuchukuliwa nyavu zao na mashine hors power 15 vifaa vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5.

Kamanda Saad amesema jeshi limefungua mashtaka na kumtafuta mtu anaedaiwa kumpiga jiwe mvuvi wa Chwaka……

Nae Sheha wa Shehia ya Chwaka Simai Msaraka Pinja akizungumza na mwandishi wetu amesema kurejea kwa ugomvi huo ni kinyume na makubaliano yaliofikiwa mbele ya rais wa Zanzibar.

Pinja ameiomba serikali kingilia kati kwa kuzuka tena mgogoro huo ulipatiwa ufumbuzi kwa kuwapatanisha wavuvi wa vijiji hivyo na kuweka mikapa ya maeneo ya uvuvi na hifadhi..

Wavuvi hao waliojeruhiwa Kassim Banzi Mgongo na Mwinyi Mwaka wamesema walivamiwa na wavuvi hao wakitumia faiba mbIli na kuchukua vifaa vyao vya uvuvi.

Wamesema hilo ni tukio la pili ndani ya kipindi cha wiki mbili cha kuvamiwa  na wavuvi wa Marumbi na kuchukua mitego yao…….

Ugomvi wa wavuvi wa vijiji vya Chwaka na Marumbi uliodumu kwa miaka mingi ulipatiwa ufumbuzi kiasi ya miaka miwili iliyopita na viongozi wa serikali akiwemo rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein kwa wavuvi kupatanishwa na kulipwa fidia za vifaa vyao vilivyoharibiwa.

20

Advertisements