Archive for January, 2015

MATOKEO YA DARASA LA SABA STD VII NA KIDATO CHA PILI YAPO HAPA

MATOKEO YA DARASA LA SABA NA KIDATU CHA PILI BONYENZA HAPA http://pembablog.blogspot.com/2014/01/matokeo-ya-kidato-cha-pili-na-darasa-la.html

Advertisements

RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA MADOGO YA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI

Rais Kikwete akimuapisha Samwel Sitta  kuwa Waziri wa Uchukuzi

Rais Kikwete akimuapisha Samwel Sitta kuwa Waziri wa Uchukuzi

Rais Jakaya kikwete ametangaza mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.

Katika uteuzi huo rais amewateua mawaziri wanane wapya pamoja na manaibu watano kuwapishwa Ikulu mjini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuteuliwa.

Akitangaza uteuzi huo Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema uteuzi huo unahusu pia kujaza nafasi mbili zilizoachwa wazi na Profesa Anna Tibaijuka Na Profesa Sospeter Muhongo.

Balozi Sefue aliwataja mawaziri hao, George Simbachawene – Waziri wa Nishati na Madini, Mary Nagu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Christopher Chiza – Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji.

Harrison Mwakyembe – Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, William Lukuvi – Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Steven Wasira – Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Samwel Sitta -Waziri wa Uchukuzi na Jenista Muhagama – Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.

Manaibu waziri walioteuliwa ni Stephen Masele – Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais – Muungano, Angela Kairuki –  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Ummy Mwalimu – Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na Anna Kilango – Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na  Charles Mwijage – Naibu Waziri wa Nishati na Madini.