Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete ameshauri kumalizwa mvutano wa kisiasa uliomo ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ili kuweka mazingira mazuri ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Octoba mwaka huu.

Akilihutubia bunge la Jamhuri ya muungano tanzainia mjini Dodoma amesema hali hiyo ya kisiasa inaweza kumalizwa endapo vyama vya CCM na CUF vilivyounda serikali hiyo vitakaa pamoja kundoa mvutano huo.

Amesema vyama hivyo vimeweza kufikia muafaka kufuatia hali mbaya ya kisiasa iliyojitokeza kabla ya kuundwa serikali hiyo hivyo iko haja ya kupatiwa ufumbuzi tofauti ziliopo ndani ya serikali.

Aidha rais Kikwete amesema katika uongozi wake serikali imefanikiwa kuyapatia ufumbuzi matatizo ya muungano 13 kati ya 15 yalioanishwa tume ya Shulukindo.

Hata hivyo amesema kero tatu zikiwemo suala la mafuta na gesi asilia kuondolewa kwenye orodha ya mambo  ya muungano zinaweza kupatiwa ufumbuzi endapo katiba inayopendekezwa itapigiwa kura ya ndio.

Wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), unaowajumisha baadhi wa wabunge wa vyama vya upinzani hawakuhudhuria katia uvunjaji wa bunge hilo.

Mwaka 2010 wakati Rais Kikwete anafungua Bunge hilo wabunge wa upinzani walisusia uzinduzi huo pia. Rais Kikwete amelivunja bunge hilo kuanzia tarehe 20 Ugust.

<!–EndFr

Advertisements