Daktari John Magufuli

Daktari John Magufuli

Chama cha Mapinduzi CCM kimemtangaza daktari John Magufuli kuwa mgombea wake wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya muungano tanzania katika uchaguzi mkuu wa octoba mwaka huu.

Daktari John Magufuli, alipata kura 2104 sawa na asilimia 87, Amina Salulm Ali alipata kura 253 sawa na asilimia 10.5 na Dk. Asha-Rose Migiro liepata kura 59.

Mpaka sasa haijafahamika nani atakuwa mgombea mwenza, lakini tetesi zilizoenea zinaashiria Amina Salum Ali ana nafasi kubwa ya kuchaguliwa kuwa mgombea mwenza kutokana na kupata ushindi wa pili.

Waziri wa mambo ya nje Bernard Membe na Naibu Waziri wa mawasiliano January Makamba walichujwa jana na halmashauri kuu kutoka orodha ya majina matano yaliyopitishwa na kamati kuu.

Kulikuwa na jumla ya wagombea 38 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo na miongoni mwa majina 33 yaliokatwa mapema ni pamoja na la Makamu wa Rais Mohamed Gharib Bilal, Waziri mkuu Mizengo Pinda na Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa.<

Advertisements